Wakati Tanzania ikipigania kuvuna Gesi asilia kutoka mikoa ya kusini,bado kumekuwa na uhaba mkubwa wa nishati. Maeneo mengi hasa ya kijijini bado wananchi wanategemea kuni kupikia. Hii imepelekea kuvuna misitu asilia hovyo.
Akinamama ambao ndio tegemezi.katika kuhudumia familia katika masuala ya chakula wamekuwa wakipata adha kubwa kutafuta kuni. Pengine ni umbali au uhaba.
Hii imeenda mbali zaidi hata kufikia hatua ya kudhuru wanafunzi ambao hupoteza muda mwingi kwenda maporini kutafuta kuni za kupikia shuleni.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako