Tuesday, 31 December 2013

SHUKRANI KWA WADAU WA BLOG HII

Wapendwa wasomaji wa blog ya Karibu Nyumbani, tunapomalizia mwaka 2013 sina budi kuwashukuru kwa usomaji wenu na yote ktk blog hii. Pia nawakaribisha mwakani. Kwaherini kutoka 2013.

KAMISHNA MPYA WA JESHI LA POLISI TANZANIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatatu, Desemba 30, 2013, amemteua Kamishna wa Polisi Ernest Mangu kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa usiku wa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue inasema kuwa Kamishna Mangu anachukua nafasi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini anayestaafu, Saidi Mwema.Kabla ya uteuzi wake unaoanza keshokutwa, Januari Mosi, 2014, Kamishna Mangu alikuwa Mkurugenzi wa Inteligensia ya Jinai*"(Director of Criminal Intelligence)"*katika Jeshi hilo la Polisi.Aidha, taarifa hiyo inasema kuwa Rais Kikwete amemteua Kamishna Abdulrahman Kaniki kuwa Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi, ambayo ni nafasi mpya katika muundo wa sasa wa Jeshi la Polisi.Kabla ya uteuzi wake, Kamishna Kaniki alikuwa Kamishna wa Uchunguzi wa Kijinai*"(Commissioner for Forensic Investigations). "*Mkuu wa Jeshi la Polisi mpya ataapishwa kesho, Jumanne,  Desemba 31, 2013 katika Viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam.

Monday, 30 December 2013

MAMBO 10 MUHIMU YA KUWAFANYIA WAZAZI/WALEZI

1. Waonyeshe umekuwa mkubwa
Biashara ya mambo ya kitoto mbele ya wazazi punguza na kama ikiwezekana hata utani wa kijingajinga usio na kichwa wala miguu achana nao. Fikiria kabla ya kuongea na ukumbuke hawa ni matured adults.

*2. Beba Majukumu na Saidia Nyumbani Ukiweza* 
Una mdogo wako anasoma lipa ada, umeshindwa nunua hata madaftari na Uniform tu. Umeona mdogo wako kamaliza shule yupo nyumbani tu mlete mjini alafu msomeshe hata ka kozi ka computer. Baba au mama anajiskia vibaya tuma nauli aje atibiwe Dar na lipa hospital Bills, misaada mingi tu unaweza fanya. Usitegemee kaka au dada zako jitahidi uwe wa kwanza wewe. e.t.c

*3. Muda* 
Tenga muda maalum wa kuwa nao, Imefika Christmass panda basi kakae nyumbani wewe na familia yako. Umepitisha wiki hujawasiliana na mama au baba mpigie simu hata kila weekend. Wafanye wajivunie kuwa wana mtoto anayewajali.

*4. Timiza Ahadi na Usidanganye* 
Hata kama maji yapo vipi shingoni kuwa mkweli kwa wazazi wako. Jitahidi ufunguke mwanzo mwisho. Wamepitia maisha na mambo mengi wanayajua zaidi yako. Umeahidi ntakupigia baadae mama jitahidi upige hiyo simu timiza ahadi. Kuna kitu huwezi fanya wajulishe na sababu utoe sio unaweka ahadi za uongo alafu ukibanwa unazidisha uongo kama mwezi huu hatujalipwa e.t.c

*5. Jitume Kwao* 
Saidia kazi za nyumbani sio unajitia busy na masomo wakati wote. Mama ana mzigo nenda mpokee sio mpaka uitwe. Kama mzazi anasafisha labda chumbani kwake achia unachofanya mshirikiane kwa pamoja. Unajua kupika saidia. Ukiwa na muda osha vyombo nyumbani.

*6. Never Say NO* 
Umetumwa nyanyuka na fanya hapo hapo. Mzazi anavyokwambia kitu ukampotezea ni jambo linaloumiza sana mioyo yao. Huwa wanahisi wamedharaulika na hujihisi wanyonge kwako. Usithubutu kupuuza hata kama wapole vipi kwako. Mara nyingi huwa hawawezi kukwambia kitu ambacho wao wanajua hukiwezi. Hivyo jibu liwe ndio wakati mwingi. Mwanangu nina shida ya hela mjibu ntakutafutia sio sitaki au siwezi.

*7. Wajulishe Hatua Unazopitia Zote* 
Umenunua kiwanja waambie wawemo kwenye furaha yako. Umemuona mchumba unataka KUMUOA mpeleke nyumbani ukamtambulishe. Umepata kazi nzuri waambie na ukihama pia wajulishe. Mke wako kashika ujauzito sema. Baki ya kwamba wazazi wengi wanafurahia sana mafanikio ya watoto wao pia Hili hujenga imani kwao kuwa unawaamini vya kutosha.

***8. Rekebisha Tofauti* 
Umekasirishwa na mzazi ongea nae kwa upole bila kupandisha sauti. Kakuonea ana hasira muache rudi baadae mueleze kinyongo chako. Kununa au kuwaongelea vibaya kwa majirani haifai. Mfano mama amekuudhi sana na una feel comfortable kwa baba basi mueleze baba linalokukera.

***9. Zawadi* 
Mama hana kanga nzuri jitoe kimasomao ndo ukubwa. Nunua hata ndala tu za mzazi kama zinaonyesha dalili ya kuisha. Zawadi ndogo ndogo ni silaha kubwa sana kwa wazazi maana huonyesha unawajali toka ukiwa na umri mdogo. Umeenda likizo nyumbani na watoto hakikisha unabeba chochote. Ukitaka kujua wazazi wanathamini sana zawadi ni wakati unarudi kwako lazima utafungashiwa tu chochote kile kwenye kiroba hata machungwa tu.

*10. Sifa* 
Mmekaa wawili na mzazi toa shukrani kwake kwa kila jema alilokutendea. Msifu kwa wema wake na umwambie kwanini unajihisi una bahati kumpata yeye kama mzazi. Kumbuka wazazi wamefanya mengi sana kwako kuliko hata unayoyajua. Usichoke kushukuru na kuwamwagia sifa. Wafanye watambue kuwa wao ni mfano mzuri sana wa kuigwa na hawajakosea hata kitu kimoja katika malezi yako. Shukrani zikiambatana na vitendo kama Kumkumbatia mama au baba wakati zinatolewa huwa zinapendeza zaidi.

Sunday, 29 December 2013

MAPUMZIKO MUHIMU

Taswira tunapoelekea kumaliza mapumziko ya mwisho wa juma. Mapumziko ni muhimu na popote. Baada ya shughuli nying halali,si vibaya kupata mapumziko kidogo. Pia tunapoelekea mwisho wa mwaka ni muhimu kutumia muda huu kupumzika huku tukipanga mikakati ya mwaka unaoanza

Saturday, 28 December 2013

MATOKEO YA DARASA LA SABA 2013

WANAFUNZI 16,482 waliofaulu mtihani wa darasa la saba mwaka huu wamekosa nafasi za kujiunga na kidato cha kwanza, kutokana na uhaba wa shule za sekondari nchini. Idadi hiyo ni kati ya wanafunzi 427,609 waliofaulu mtihani huo uliofanyika Septemba 11, katika maeneo mbalimbali nchini, ambapo wanafunzi 411,127 wamechaguliwa kujiunga na sekondari. Matokeo hayo yalitangazwa jana jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini, wakati akizungumza na waandishi wa habari.  Sagini alisema wanafunzi waliokosa nafasi wanatoka katika mikoa minane, ikiongozwa na Dar es Salaam yenye wanafunzi 11,796, Mbeya 1,484, Geita 1,578, Dodoma 549, Njombe 379, Morogoro 315, Katavi 261 na Mtwara 120.  Alisema wanafunzi waliokosa nafasi watasubiri hadi Februari mwakani, iwapo watapata shule katika uchaguzi wa awamu ya pili, kutokana na baadhi ya wanafunzi kwenda katika shule binafsi.

Friday, 27 December 2013

HAMU YA UTAJIRI WA HARAKA WAMPONZA JAMANI

Dada huyu wa Kitanzania akamatwa china akiwa na madawa ya kulevya. A 28-year-old woman from Tanzania was arrested on a charge of drug possession in Macao, Dec 19, 2013. She hid 1.1 kilograms ofheroin valued at $137,720 in her body and took a flight from Thailand to Macao on Tuesday. She said her destination was Guangzhou, capital of South China's Guangdong province.

VIOJA KWENYE DALADALA

Wadau bila shaka mlikuwa na xmasi njema. Sasa tunarudi tena kwenye majukumu kabla ya kufunga mwaka. Lakini tujikumbushe vioja hivi tunavyokumbana navyo kila siku.


Mlokole: "Nyimbo gani mnapiga?!?
Wekeni nyimbo za Yesu.."
Konda: "Vipi wewe, Yesu bado
hajatoa album...

Abiria: "Kuna Kiti au unasema
panda tu!?"
Konda: "hao wengine wamekalia
ndoo?! "

Abiria: "Embu punguzeni sauti ya
redio..."
Konda: "Sheria za nchi tu
zinatushinda, tusikilize na zako!?
hebu tupunguzie misheria"

Mmama: "Bwana ondoa gari joto
sana!!"
Konda: "Usituzingue wewe,
shuka upande fridge...."

Konda: "Anti, kuna siti pale
nyuma,ingia...."
Anti: "Siwezi kaa siti za nyuma..."
Konda: "Kwani za nyuma ziko nje ya gari?!"

Sister duu: "Konda unanibana
bwana..."
Konda: "mbona nguo ulizovaa
huzisemi, kama ulitaka kujiachia
ungekodi treni peke yako

Sharobaro: "Kuna kiti?! Kama
hamna sipandi..."
Konda: "Kama unaogopa kukosa
kiti si ungebeba chako!!?"

Thursday, 26 December 2013

Umbea kidogo: DIAMOND PLATNUMZ

Mwanamuziki Diamond akipagawisha watazamaji wake jana ktk viwanja vya Leaders Club Mwanamuziki Diamond akicheza na mpenzi wake wa zamani Wema Sepetu;ambapo fununu za kurudiana zimeenea mjini. Baada ya Tamasha hilo la Leaders Club. Diamond na jopo lake la Wasafi Classic walikwea "private jet" kuelekea Mwanza kwa tamasha la leo Boxing Day.

Wednesday, 25 December 2013

INAPENDEZA: WATU NA TAASISI MBALIMBALI WASHEREHRKEA XMAS.KWA KUTOA MISAADA KWA VITUO VYA

Kiongozi wa wanafunzi wa CBE-Dodoma akikabidhi zawadi kituo cha Miyuji huko Dodoma Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa akitoa msaada kwa kituo huko Bigwa-Morogoro Meya wa Manispaa ya Kinondoni akikabidhi zawadi

MERRY XMAS/KHERI YA KRISMASI WADAU

Wakati Wakristo pote duniani wanajumuika pamoja kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa Yesu; nawatakia wapendwa wote wa blog hii na watu wote Heri ya Krismasi. Tuisherehekee kwa furaha na amani maana ni mfalme wa amani amezaliwa.

Tuesday, 24 December 2013

KITUO CHA POLISI OYSTERBAY KUVUNJWA KUPISHA UJENZI WA MADUKA YA KISASA

* Kituo cha Polisi cha Oysterbay, pamoja na nyumba za Polisi wanaoishi katika Kambi hiyo, vitabomolewa kwa ajili ya kupisha ujenzi wa maduka ya kisasa mfano wa Mlimani City ujenzi unaotarajia kuanza mwakani.**
** Tayari baadhi ya askari waliokuwa wakiishi katika Kambi hiyo wameshapewa 'Notis' ili kuhama katika nyumba zao na wengine kubomoa wenyewe majengo waliyokuwa wamejengwa kwa mabati katikati ya kambi hiyo ambayo walikuwa wakiishi, ambapo wengi wao waliokuwa wakiisha katika nyumba za mabati wamekwishabomoa nyumba zao na kuhama, huku baadhi wakiwa wamesalia wakisubiri awamu ya pili. Askari hao wameelekezwa kuhamia katika nyumba mpya zinazojengwa eneo la Kunduchi.**
**Baadhi ya askari wamelalamikia utaratibu huo wa kuhamishwa katika eneo hilo, hali ya kuwa pamoja na kubomolewa nyumba zao na Kituo cha Polisi, lakini imeelezwa kuwa kitajengwa Kituo kipya kikubwa katika eneo hilo ambacho kitajengea upande wa pili barabara ya Ubalozi wa Marekani.**
**Kinachowafanya baadhi ya askari kulalamikia utaratibu huo ni kutokana na kujengwa tena kituo kikubwa katika eneo hilo, lakini nyumba za askari zikiondolewa na kutotakiwa kuwepo tena, ambapo askari wote watapewa nyumba Kunduchi na kila atakayekuwa zamu atalazimika kusafiri ili kufika kazini, jambo ambalo limeonekana ni usumbufu na hasa pale itakapotokea dharula za kikazi.*

TUSICHEZEE ZAWADI YA UHAI

Wakati wenzetu wa Africa Kati na Sudan Kusini wanatapatapa kwa vita,hawa wenzetu na sisi nao wanajaribu Bomu bandia lao. Uuuuuh kila mtu kapewa akili zake jamani. Onyo: Tafadhali usijaribu hii

Monday, 23 December 2013

HAPA MMOJA ATAAMKIA MUHIMBILI NA MWINGINE SEGEREA."TIMBWILI"

Mama mkwe kamkuta jamaa sebuleni kapandisha hasira anadai ataua mtu.
*MAMKWE*: Mwanangu kwani kuna nini jamani?
*MJAMAA*: Leo namuua mwanao, mshenzi sana?
*MAMKWE*: Tulia jamani kimetokea nini?
*MJAMAA*: Mwanao mshenzi nilikuwa nimesafiri, nikamtumia meseji kuwa nakuja, hajajibu; eti bado leo nimefika nimemkuta na mwanaume kwenye kitanda chetu dharau gani hii, sikubali leo tunagawana majengo ya serikali, yeye anaenda kulala Muhimbili mi naenda kulala Segerea
*MAMKWE*: Subiri kwanza mwanangu hayuko hivyo lazima kuna maelezo fulani kuhusu hili ngoja nimuulize...mama mkwe akamfuata mwanawe na baada ya muda akarudi sebuleni
*MAMKWE*: Unaona, nilijua mimi lazima kuna sababu. Kumbe mwenzio hakupata ile meseji uliyomtumia.

NAWATAKIA WIKI NJEMA

Tunapoinza wiki hii yenye pilika nyingi; wengine wanawahi kwenye majukumu yao. Wengine ndo maandalizi ya sikukuu ya Xmasi kimanunuzi. Pengine wengine wapo safarini. Na kila mmoja pale alipo kwa namna yake;nyote nawatakieni iwe wiki njema yenye furaha na amani tele

Saturday, 21 December 2013

TUACHE KUKURUPUKA KWENYE MAAMUZI.

POKEA NASAHA:
BABA 1 alikuwa anaosha gari lake jipya, MWANAE mdogo wa miaka 5 akalichora hilo gari ubavuni kwa jiwe. BABA akakurupuka na kumbana mkono kwa koleo,ikapelekea vidole 3 kuharibika. Wakiwa hospitali, wakati anakatwa vidole, MTOTO akamuangalia BABA, akamuliza, vitarudi tena? BABA akaumia sana, akarudi kwenye gari aone MTOTO alivyochora, Kakuta MTOTO kaandika, DADY, I  LOVE YOU. Kanuni ya maisha ni WATU wapendwe, VITU vitumiwe. Tatizo la walimwengu wa leo, wanapenda VITU, kuliko WATU. Kumbuka neno la MUNGU lasema,  "PENDANENI KAMA NINAVYOWAPENDA MIMI"

Mhe.ZITO KABWE APOKELEWA KISHUJAA KIGOMA. Kweli nyumbani ni nyumbani

Mhe.Zito Kabwe akiwa katika gari la wazi kuwasalimu wananchi wa Kigoma Wananchi waliojitokeza kumlaki mbunge wao mhe.Zito Kabwe

Friday, 20 December 2013

BREAKING NEWS:MAWAZIRI 4 KUTENGULIWA VYEO VYAO

 Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda amesema kwamba Rais Kikwete amekubali kutengua nyadhifa za mawaziri wanne kufuatia ripoti ya 'Operesheni Tokomeza' iliyotolewa mapema leo bungeni.  Mawaziri hao waliotenguliwa nyadhifa zao ni: Mhe. David Mathayo David wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Khamis Kagasheki wa Maliasili na Utalii, Mhe. Emmanuel Nchimbi wa Mambo ya Ndani na Mhe. Shamsi Vuai Nahodha wa Ulinzi.  Mhe. Kagasheki alitangaza kujiuzulu mapema kabla uamuzi huo uliotangazwa na Waziri Mkuu. Waziri wa Maliasili na Utalii: mhe. kagasheki Waziri wa Mifugo na Uvuvi:mhe. David Matayo David Waziri wa Mambo ya Ndani mhe. Emanuel Nchimbi Waziri wa Ulinzi na JKT mhe. Shamsi Vuai Nahodha

UWANJA WA AMANI ZANZIBAR WAFANYIWA MAREKEBISHO NA KUWEKEWA NYASI BANDIA

Uwanja huo unavyoonekana kwa sasa. *Uwanja wa Amani wa Zanzibar maarufu kama Amani Stadium umefanyiwa marekebisho na kuwekewa nyasi bandia.**Baada ya kukamilika ulifanyiwa majaribio kwa mechi ya vijana wa mika chini ya 20** **Hii ni katika maandalizi ya sherehe za mapinduzi. Uwanja huo umekuwa wa kisasa zaidi kwa wakati huu.* Uwanja huo ktk kipindi cha ukarabati

TUWE WATU WA SHUKRANI

Ni katika pilikapilika za maisha ambapo wengi hujifunga mkanda katika majukumu yao kutafuta chochote kwa ajili yao na familia. Lakini mara nyingi hujinyima sana ili mambo yaende au kumridhisha mke/mume au familia. Lakini ni mara ngapi tunashukuru huduma hizo? Yeye anapopiga ugali kwa maharage wewe umeletewa hiki bado walalamika. Tujitahd kushukuru kwa chochote

TASWIRA ZA TRENI KATIKA NCHI MBALIMBALI

Treni nchini Tanzania Treni nchini Nigeria Treni nchini India Treni nchini Marekani (USA) Treni nchini Uingereza Treni nchini Japan na china Treni nchini Ujerumani Treni mahali fulani

TOZO YA KODI KWA LINE ZA SIMU

Habari za kodi kwa laini za simu ilichukua vichwa vya habari kwa wakati wake hadi pale mheshimiwa Rais alivyotoa agizo kwa wahusika kulishughulikia hili suala. Naibu Waziri mwenye dhamana ya mawasiliano,sayansi na teknolojia “January Makamba” ametoa habari mpya na nzuri  kuhusu kodi hii. Kupita ukurasa wake wa facebook alipost “Mheshimiwa Rais ametia sahihi Hati ya Dharura (Certificate of Emergency) kufanyika marekebisho kwa Muswada wa Fedha wa mwaka 2013 kuondoa tozo ya kodi kwa laini za simu (SimCard Tax). Asante Mheshimiwa Rais.”.

Tulikotoka ni mbali

Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo. Mama huyu naona kaamua kumwonyesha mwanae maisha yalivyo Watoto hawa pia japo wafurahia mazingira ya nyumbani ila pia wanajiandaa kuwa wanamichezo wazuri hapo baadae. Muhimu ni kukuza tu vipaji vyao Huyu nae ametokelezea kivyake alivyokuwa anacheza. Ama kweli nyumbani raha

Wednesday, 18 December 2013

Mv.MAGOGONI chapata kizaazaa leo

Kivuko kikubwa cha MV Magogoni leo kimekwama katikati ya bahari katika Bandari ya Dar es Salaam kutokana na hitilafu za kiufundi.Pantoni hilo linafanya safari kati ya Kigamboni na Magogoni, Dar es Salaam. Kiini cha kizaazaa hicho bado hakijafahamika, ila mashuhuda wanasema  Kivuko kilipoteza mwelekeo majini  kikiwa na abiria na magari baada ya injini zake kushindwa kufanya kazi. *" Juu abiria wanaonekana wamevaa "life jackets" ikiwa itatokea kupiga mbizi au la. Chini ni mv.Magogoni inavyoonekana ktk safari zake kawaida

Ndege ya shirika la Ethiopian Airline yatua Arusha kwa dharura

Habari iliyoifikia hivi punde toka jijini Arusha, inaeleza kuwa Ndege ya abiria aina ya Boeing 787 ya shirika la ndege la Ethiopia (Ethiopian Airlines) mchana huu imeshindwa kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kutoka na hitilafu iliyokuwepo Uwanjani hapo na kulazimika kutua kwa dharula kwenye Uwanja wa Mdogo wa Arusha,hali iliyopelekea Ndege hiyo kusimama nje kabisa ya uwanja huo huku abiria zaidi ya 200 wakiwa ndani ya ndege hiyo mpaka sasa bila ya kushuka.**** ****Wataalam wa Ndege wapo eneo la tukio hivi sasa kutafakari namna watakavyoweza kuwashusha abiria hao na kutafuta namna ya kuweka sawa mambo ili Ndege hiyo iweze kuruka.**** ****Tuinaendelea kufatilia kwa ukaribu tukio hilo, na tutaendelea kufahamishana kadri taarifa zitakavyokuwa zinakitufikia.* * **PICHA NA MDAU WETU KUTOKA ARUSHA*