Sunday, 15 December 2013
Hatimaye Mandela azikwa huko Qunu
Leo ndio siku ya mazishi ya Mwana wa Mama Afrika, Nelson Rolihlahla Mandela. Anazikwa kijijini kwao Qunu.
Mandela anayetoka kwenye kabila la Xhosa alizaliwa Julai 18, 1918 kijijini Mvezo, kando ya mto Mbashe, Wilaya ya Umtata, Makao Makuu ya Jimbo la Transkei.
Ukoo wa Mandela una mahusiano na Ukoo wa Kifalme wa Thembu. Baba yake Mandela, Gadla Henry Mphakanyiswa alikuwa Chifu kwa damu na kwa desturi. Naye akathibitishwa kuwa Chifu wa Mvezo na Mfalme wa himaya ya Thembu.
Mandela mwenyewe alizaliwa na jina Rolihlahla, ikiwa na maana ' Mwenye kuvuta matawi ya miti'. Na kwa lugha yao ina maana ya ' Msumbufu'.
Na hakika, Mandela amekuwa ' Msumbufu' kwa utawala wa kibaguzi hadi pale waliposalimu amri.
Mandela anasimulia, kuwa kumekuwa na hekaya sizizo za kweli kwenye kabila lao, kuwa naye ( Mandela) alikuwa mmojawapo katika mlolongo wa kurithishwa Uchifu kwenye himaya ya Thembu. Kwamba ingefika wakati naye Mandela angetawazwa kuwa Chifu. Mandela analikanusha hilo, anasema;(P.T)
Juu mwili wa Mandela ukiwa juu ya kaburi tayari kuzikwa.
Chini ni mama Vicky Swai(aliyetunza viatu vya Mandela akiwa Tanzania) na mama Maria Nyerere katika mazishi ya Mandela huko Qunu
No comments:
Post a Comment
Maoni yako