Kijana huyu anapita katikati ya mitaa ya jiji ya Dar akiuza manati. Nijuavyo mimi manati inatumika zaidi kuwindia ndege kwa ajili ya kitoweo au kufukuza wasiharibu mazao. Sasa najiuliza, manati inauzwa jijini kwa ajili ya kuwindia nini? Na hapa nakumbuka ule msemo wa "usitupe mawe kwenye nyumba zenye madirisha ya vioo". Kwa ushauri wangu, biashara kama hii ingefaa sana maeneo wanayolima mpunga,ngano na ulezi (vijijini) ambapo matumizi yake yangeenda sawia na hali ya mazingira.Tusijelalamika, jijini sipati wateja kabisa wa bidhaa zangu!,uliangalia upatikanaji wa soko hilo kabla hujaanza hiyo biashara?
No comments:
Post a Comment
Maoni yako