Mpendwa,
Nakuomba usichoke kuisoma hadithi hii,inafundisha sana,nawe upate kujifunza kitu katika hadithi hii...Fuata basi na ahsante kwa kuisoma na kutoa maoni wewe waonaje?
Kaka Chongo alikuwa akimchukia sana babake, kisa alikuwa chongo…
Baba yake alikuwa anafanya kazi ya ualimu na kufanya biashara ndogondogo ili kuweza kumtunza mtoto wake pekee. Mtoto ambaye alikuwa akimsomesha shule ya bweni kule Tabora. Baba huyu alikuwa "mjane", mkewe alifariki kwenye ajali ya gari, miaka mingi nyuma....
Siku moja alifunga safari kwenda kumtembelea mtoto wake kule shuleni. Mtoto wake hakufurahia ujio wa Baba yake, na chuki yake ilionekana dhahiri kuwa amechukia.
"Kwanini huyu mwanaume anapenda kuja kuniaibisha kila mara," alijisemea moyoni, dharau zake kwa baba yake na kutojali kwake kulionekana wazi wazi usoni kwake.
Siku ya pili yake mwanafunzi mwenzake darasani alimuuliza… “kumbe wewe Baba yako anajicho moja?” kijana yule akamjibu yule si Baba yangu, ni jirani yetu kule nyumbani...
Kwa kweli hakumpenda Baba yake... alitamani apotelee mbali asimuone tena...
Au afe asiwepo tena duniani...
Baba yake hakumchukia na wala hakuonyesha kisirani kwa mtoto wake…
Kijana yule alisoma kwa bidii sana ili aweze kupata scholarship, ili atakapopata nafasi yakuendelea na masomo ya juu,awe mbali na Baba yake…
Kwa bidii zake alifanikiwa kwenda kusoma nje ya nchi kwa miaka mitatu…
Kwa miaka yote hiyo hakuwahi kuwasiliana na baba yake, na watu wakimuuliza kuhusu wazazi wake aliwajibu kuwa walishafariki siku nyingi…
Baada ya kumaliza masomo nje ya nchi, alirejea nchini na kununua nyumba, akaoa na baada ya miaka michache akapata watoto wawili… Akawa ni mtu mwenye furaha na maisha yake na familia yake…
Siku moja Baba yake ambaye sasa ashakuwa mzee sana, akaja kumtembelea, baada ya kuitafuta nyumba yake kwa takribani siku nne... Baba yake alikuwa ametamani kumuona mwanaye kabla M’Mungu ajamchukuwa… Na pia alitamani kuwaona wajukuu zake…maana alisikia habari hizo.
Alipokuwa akigonga mlango, wakatoka wajukuu zake… walipomuona kibabu kizee chenye jicho moja wakacheka na kumwambia baba yao… kuna omba omba kaja anaonekana ana njaa sana huku wakicheka… Mwanaye alipotoka kumuona huyo omba omba, akagunduwa kuwa si ombaomba bali ni Baba yake mzazi…
Alimwangalia kwa jicho kali na dharau na huku akimkaripia… hivi wewe kizee ujafa tuu…. Na umekuja kufanya nini hapa unatisha watoto wangu… Toka nisikuone hapa hatuna chakula wala pesa za kukupa…. Yule Baba akajibu kwa upole... “Samahani baba nimekosea nyumba nilifikiri hapa anaishi mtoto wangu Fulani…!! Kijana akajibu huna mtoto nyumba hii huna haya weee mzee…!!
Yule Baba huku akilia ndani ya nafsi yake akajiondokea taratibu huku akijikongoja kwa uzee…
Wiki chache kupita, kijana akaletewa barua kutoka kwa wakili wa serikali. Wakili akamtaka aende ofisini kwake. Alipofika na kujitambulisha, wakili akamfahamisha kuwa Baba yake ambaye alikuwa analelewa nyumba ya wazee amefariki siku tatu nyuma. Akampatia na barua kutoka kwa Baba yake. Wakili akashangaa kwani kijana hakuonyesha hata kusikitika…!!
Habari ya kufiwa haikumuuzunisha hata chembe…
Aliporudi nyumbani akajifungia ndani peke yake na kuisoma barua hile...
Kwa mwanangu mpendwa...
Siku zote nilikuwa nakufikiria na kukuombea dua ufanikiwe...
Nakutaka msamaha sana kwa kuja nyumbani kwako na kusababisha kutishika kwa watoto wako, kwa kuwa mimi nilikuwa chongo...!! Na pia nakutaka msamaha kwa vijana wote waliokuwa wakikutania kwa kuwa na Baba ambaye ni chongo...
Mwanangu mpendwa..... Tangu siku ile nilipokuja kwako, nilipata maradhi na sikuweza tena kutoka nje...!! Nawashukuru sana hawa vijana wanaotutunza hapa kwenye nyumba ya wazee...!! kwa kuweza kututunza vyema... Mwanangu mpendwa... kuna jambo moja ambalo nililificha miaka yote hii na leo nimeona nikuandikie hii barua kukufahamisha kile kilicho kuwa ni siri yangu...!!
Japokuwa utapokuwa ukiisoma barua hii... nitakuwa nimeshatangulia kwa Mola wangu...
Ulipokuwa mdogo ulipata ajali mwanangu.... wewe na Mama yako. Mama yako alipoteza maisha kwenye ajali hiyo, na wewe ukapoteza jicho lako moja...
Mimi nikiwa ni Baba yako sikufurahia kukuona ukiwa na jicho moja...
Lakini sikuwa najinsi ya kufanya... Lakini nilijitahidi kutafuta pesa na nikachukua mkopo serikalini nikakupeleka nje ya nchi kufanyiwa operesheni ya jicho...!! Nikakubali kutolewa jicho langu moja kukupa wewe mwanangu ili uione dunia kwa macho mawili… uwe ni mwenye furaha duniani na kukuepusha kuchekwa na watoto wenzio....
Wenzangu walishangaa sana kusikia kuwa nimetoa jicho langu kwa ajili yako mwanangu... lakini najivunia tendo langu hilo kwani ni tendo ambalo limenipa furaha ktk maisha yangu kwa kumwona mwanangu anakuwa na furaha ya kuona ulimwengu akiwa na macho yote.
With my love to you… huo ni urithi pekee nilioweza kukupatia…
Ndimi Baba yako….
Mzee Chongo
Tusiwasahau wote maana hatujui tumetendewa nini mpaka tukafika hatua tuliyo nayo
No comments:
Post a Comment
Maoni yako