Tuesday, 28 March 2017

SOKO LA KARIAKOO ZAMANI NA SASA

Soko la Kariakoo mwaka 1974
Soko la Kariakoo leo mchana 28 Machi,2017

Monday, 27 March 2017

NEY WA MITEGO AACHIWA: WIMBO WAKE RUKSA KUPIGWA

Msanii Ney wa Mitego ameachiwa huru na kushauriwa Wimbo wake huo ikiwezekana aufanyie marekebisho kuongeza vitu mbalimbali na kuendelea kupigwa. Hayo yamesemwa na mhe Harrison Mwakyembe akitoa ujumbe toka kwa Mhe rais Magufuli kuhusu kukamatwa kwa Ney na wimbo wake kufungiwa na BASATA.

Wimbo wake usikilize hapa chini;

Sunday, 26 March 2017

UTEUZI: MAKATIBU WA CCM MIKOANI

1 Arusha - Elias Mpanda


2 Dar - Saad Kusilawe
3 Dodoma - Jamila Yusuf
4 Geita - Adam Ngalawa
5 Iringa - Christopher Magala
6. Kagera- Rahel Degeleke
7. Katavi- Kajoro Vyahoroka
8. Kigoma- Naomi Kapambala
9. Kilimanjaro- Jonathan Mabihya
10. Lindi-Mwanamasoud Pazi
11. Manyara -Paza Mwamlima
12. Mara -Innocent Nanzabar
13. Mbeya -Wilson Nkhambaku
14. Morogoro- Kulwa Milonge
15. Mtwara -Zacharia Mwansasu
16. Mwanza- Raymond Mwangala
17. Njombe- Hossea Mpagike
18. Pwani- Anastanzia Amasi
19. Rukwa- Loth Ole Nesere
20. Ruvuma- Amina Imbo
21. Shinyanga -Haula Kachambwa
22. Simiyu- Donald Etamya
23. Singida- Jimson Mhagama
24. Tabora- Janeth Kayanda
25. Tanga- Allan Kingazi.

NAY WA MITEGO AKAMATWA NA POLISI HUKO MOROGORO

Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro, Kamanda Ulrich Matei amethibitisha kukamatwa kwa msanii Nay wa Mitego usiku wa kuamkia leo mkoani Morogoro.

Kamanda Ulrich Matei ametoa sababu kubwa ya kukamatwa kwa msanii huyo ni kutokana na kutoa wimbo unaofahamika kwa jina la 'Wapo' ambao anadai unaikashfu Serikali iliyopo maradakani.

Kamanda Matei amesema shauri la Nay wa Mitego lipo jijini Dar es Salaam hivyo msanii huyo atasafirishwa na kupelekwa Dar es Salaam kuhojiwa kwa Mkuu wa Upelelezi wa mkoa.

Saturday, 25 March 2017

HAWATAKI MCHEZO WA CHIPS ZA KUPIMIWA

hapa ni kula ushindwe mwenyewe
Hizi za kupimiwa sijui kama hawa hapa chini zitawahusu

UTEUZI: KAMISHNA MKUU WA TRA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 25 Machi, 2017 amemteua Bw. Charles Edward Kichere kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Kabla ya Uteuzi huo Bw. Charles Edward Kichere alikuwa Naibu Kamishna Mkuu wa TRA.

Bw. Charles Edward Kichere anachukua nafasi ya Bw. Alphayo Kidata ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu, Ikulu.

Kufuatia uteuzi huo, nafasi ya Naibu Kamishna Mkuu wa TRA itajazwa baadaye.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

25 Machi, 2017

MHE NAPE NNAUYE ATENGULIWA UWAZIRI

Nape Nnauye amezungumza na Waandishi wa habari akiwa juu ya gari lake leo maeneo ya St. Peter Osterbay Dar es salaam ikiwa ni saa chache kabla ya taarifa kutoka IKULU kutangaza kwamba nafasi yake ya Waziri wa Habari amepewa Dr. Mwakyembe, hii ni Sentensi hapa chini ya jinsi ilivyokua


"Nataka aliyeinua bastola hapa aje aseme ameiinua kwa sababu gani" - Nape Nnauye


"Nia ya mkutano wangu haikuwa mbaya. Nilitaka kuzungumza na waandishi wa habari lakini Polisi wanakuja kunizuia."- Nape


"We have nothing to fear, but fear itself."- Nape


"Mnajua ni kiasi gani nimepigana kuirudisha CCM madarakani? Miezi 28 nimelala porini leo mtu anakuja kunitolea bastola. Jana nilisema kuwa kuna gharama za kulipa wakati unatetea haki za watu. Na nilisema kuwa nipo tayari kuilipa gharama hiyo. Sina kinyongo na serikali wala chama changu. Sikumuuliza Rais siku aliniteua na sitamlaumu kwa kuamua kuniondoa."- Nape


"Niliikuta CCM iko shimoni nikaitoa huko. Uzalendo wangu ndani wa CCM si wa kutiliwa shaka. Kina Kawawa walikuwepo wakapita, sisi tutapita, lakini tujiulize tutawaachia watoto wetu Tanzania ya namna gani?"- Nape


"Namshukuru Rais kwa mwaka mmoja alioniamini. Nampongeza kaka yangu Dkt Mwakyembe. Nawaomba mumuunge mkono Waziri Mwakyembe. Nawaomba mtulie maisha yaendelee. Nape ni mdogo sana kuliko nchi. Kuna mambo mazuri mbele hivyo tuiunge mkono serikali."- Nape


"Vijana naomba msimamie haki yenu"- Mbunge Nape Nnauye


"Mimi niliwahi kufukuzwa CCM kwa kusimamia nilichokiamini. Ili mbegu iote na kuchanua, sharti ioze kwanza."- Nape


"Namshukuru Rais kwa mwaka mmoja alioniamini. Nampongeza kaka yangu Dkt Mwakyembe. Nawaomba mumuunge mkono Waziri Mwakyembe. Nawaomba mtulie maisha yaendelee. Nape ni mdogo sana kuliko nchi. Kuna mambo mazuri mbele hivyo tuiunge mkono serikali."- Nape


"Nilitamani sana kuendelea kufanya kazi na ninyi waandishi wa habari lakini muda wa aliyeniweka umefika akaamua niondoke."-Nape


"Mimi niliwahi kufukuzwa CCM kwa kusimamia nilichokiamini. Ili mbegu iote na kuchanua, sharti ioze kwanza."- Nape

Monday, 20 March 2017

UBUNGO INTERCHANGE YAWEKEWA JIWE LA MSINGI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akivuta kitambaa pamoja na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim kuashiria uwekaji wa jiwe la Msingi katika Mradi wa ujenzi wa Makutano ya barabara za Juu Ubungo Interchange jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim wakimsikiliza Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS Mhandisi Crispianus Ako aliyekuwa akielezea nama ya ujenzi huo makutano ya barabara za juu za Ubungo(Ubungo interchange) zitakavyokuwa.

MHE RAIS MAGUFULI AMSISITIZA MKUU WA MKOA KUCHAPA KAZI

Tofauti na kile ambacho watanzania wengi leo walikuwa wakitarajia kuona Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli akichukua uamuzi mgumu dhidi ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, mkuu huyo wa nchi amemuelezea Makonda kuchapa kazi.

Makonda anakabiliwa na kashfa lukuki ikiwemo ile ya kudaiwa kughushi vyeti na kwamba jina lake halisi ni Daudi Bashite, kutumia vibaya madaraka yake ikiwemo tukio la juzi la kuvamia studio za Clouds Media Group akiwa na wanajeshi wenye silaha akilamizimisha kurushwa kwa kipindi na zingine. Tukio hilo limelaaniwa vikali.

Akizungumza Jumatatu hii kwenye uwekaji jiwe la msingi katika mradi wa barabara za juu (Flyovers) Ubungo, Dar, Rais Magufuli amesema, “Mimi ndio najua mwenyewe nani anatakiwa kuwa wapi akae wapi, ni mimi ninayepanga. Ninajua wamenielewa. Kwahiyo Makonda wewe chapakazi, nasema chapa kazi.”

“Suala la kuandikwa kwenye mitandao sio tija kwangu, hata mimi ninaandikwa kwenye mitandao kwahiyo nijiuzulu urais? Chapa kazi, hapa kazi tu.”

Rais amesema Watanzania wanapoteza muda mwingi kwa mambo yasiyo ya msingi.

“Tumepoteza direction tumeanza kujadili personalities,” aliongeza.

Sunday, 19 March 2017

KIVUKO KIPYA CHA MV.KAZI

Kivuko cha MV KAZI kikielea majini baada ya kushushwa kwa mara ya kwanza tayari kwa kufanyiwa ukaguzi wa mwisho kabla ya kuanza kazi. Kivuko hicho kitakua kikitoa huduma zake kati ya Magogoni na Kigamboni na kitakua na uwezo wa kubeba abiria 800 na magari 22 kwa wakati mmoja.

MHE TUNDU LISSU, ACHAGULIWA KUWA RAIS MPYA WA TLS

Wajumbe wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), leo wamefanya uchaguzi wa kumchagua rais pamoja na wajumbe wa ngazi mbalimbali za uongozi wa chama chao.

Uchaguzi huo umefanyika mjini Arusha ambako wanachama wa TLS wamekutana kutekeleza ratiba hiyo pamoja na kupanga mipango mbalimbali ya utendaji kazi wa chama hicho.

Matokeo ni kama ifuatavyo:

Urais: Kura zilizopigwa 1682
Tundu Lissu 1411 sawa na asilimia 88
Francis Stolla 64
Victoria Mandari 176
Godwin Mwapongo 64
==>Kwa upande wa nafasi ya Makamu wa Rais (TLS) mshindi ni Godwin Ngwilimi aliyekuwa Mwanasheria wa Tanesco na kutimuliwa kwa kupinga Escrow.

Council Members
Jeremiah Motebesya
Gida Lambaji
Hussein Mtembwa
Aisha Sinda
Steven Axweso
David Shilatu
Daniel Bushele

RAIS MSTAAFU AZINDUA JAKAYA MRISHO KIKWETE FOUNDATION

Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete (kulia), akizungumza alipokuwa akizindua rasmi Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) ikiwa ni sehemu pia ya uzinduzi wa taasisi hiyo kwenye Hoteli ya Hyatt (Zamani Kempinski The Kilimanjaro) Jijini Dar es Salaam.

Taasisi ya Maendeleo ya Jakaya Mrisho Kikwete (JMKF).Taasisi hiyo imeundwa ili kusaidia Tanzania na Afrika katika kuimarisha amani, afya, utawala bora na maendeleo endelevu.Hawa ndo wajumbe 9 wa Bodi ya Wadhamini ya kwanza ya Taasisi hiyo.

Sunday, 12 March 2017

CCM "KIMENUKA"

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM taifa ambaye pia ni mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Sophia Simba na wenyeviti wa CCM wa mikoa minne wamefukuzwa uanachama wa chama hicho kwa madai ya ukiukwaji wa maadili ya chama

Mbali na maamuzi hayo, chama hicho pia kimewafukuza uanachama wenyeviti wanne wa mikoa ambao ni pamoja na Ramadhan Madabida (Dar es Salaam), Jesca Msambatavangu (Iringa), Erasto Kwilasa na Christopher Sanya (Mara).

Pia chama hicho kimetangaza kuwavua uanachama wenyeviti wake katika wilaya za Gairo, Babati Mjini, Kinondoni na Longido huku wengine wakipewa onyo kali huku.

Panga hilo pia limefika katika wajumbe wa NEC ambapo ndugu Ali Hera Sumaye kutoka Babati Mjini naye akifukuzwa uanachama na wengine kupewa onyo kali.

Maamuzi hayo yamefanywa katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho (NEC) kilichokaa leo mjini Dodoma kuelekea mkutano mkuu maalum wa chama hicho utakaofanyika kesho JUmapili ya Machi 12, 2017.

Akizungumza na wanahabari mjini humo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Humphrey Polepole ametaja maamuzi mengine kuwa ni kutoa onyo kali kwa mjumbe wake wa Kamati Kuu, Dkt. Emmanuel Nchimbi ambaye ni balozi wa Tanzania nchini Brazil, huku Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa akisamehewa

"Ndugu Kimbisa amesamehewa makosa baada ya kuomba radhi, kujirekebisha na kuwaongoza vyema wana CCM mkoa wa Dodoma kupata ushindi wa uchaguzi mkuu, Ndugu. Emmanuel Nchimbi amepewa onyo kali na anatakiwa kuomba radhi wanachama na uongozi wa CCM, tunajua huyu ni Balozi wetu Brazil, lakini ametakiwa afanye hivyo mara moja akiwa huko huko Brazil, na taarifa yetu ataipata" Amesema Polepole

Polepole amesema maamuzi hayo ni ya mwisho, na hayatakuwa na nafasi ya kukatiwa rufaa katika ngazi yoyote ya chama hicho.

Friday, 10 March 2017

MATUMIZI MAZURI NA SAHIHI YA KODI ZA WATANZANIA

Ujenzi wa majengo 20 yenye uwezo wa kuhudumia zaidi ya wanafunzi 3,840 wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo kila jengo lina ghorofa nne umekamilika baada ya kuchukua muda wa miezi minane

Thursday, 9 March 2017

MAJANGA YA SIMU ZA MKONONI KWA JAMII

Zamani kidogo ilikuwa kawaida watu wanatembeleana kujuliana hali na kujenga ukaribu kwa kushirikisha hili na lile kwa maongezi ya ana kwa ana. Pia ilikuwa kawaida kushiriki hata milo pamoja huku mkiendelea kuongea. Lakini miaka ya hivi karibuni kutokana na maendeleo ya sayansi na Tekinolojia,imeonekana yatosha t kupiga simu au ujumbe kumsalimia mtu mwingine hata zaidi ya mwaka/miaka bila kuonana. Hii yawezekana ni nzuri kwa kuokoa muda lakini binadamu kama binadamu yapendeza mnapoonana ana kwa ana

Wednesday, 8 March 2017

SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

Kila ifikapo Machi 8 ya kila mwaka, wanawake duniani kote huadhimisha siku yao ambapo hujitathmini kupitia shughuli mbalimbali za maendeleo walizofanya, changamoto zilizopo na kuweka mikakati ya utatuzi wa changamoto hizo.

Friday, 3 March 2017

HATIMAE MHE MBUNGE GODBLESS LEMA AACHIWA KWA DHAMANA

Hatimaye Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imemuachia kwa dhamana Mbunge wa Arusha Mjini kupitia CHADEMA, Godbless Lema baada ya kusota gerezani kwa zaidi ya miezi minne. Mahakama hiyo imefikia uamuzi huo baada ya kupitia hoja za pande zote mbili zilizowasilishwa mahakamani hapo leo na kuamua kuzitupitilia mbali hoja za upande wa serikali za kumnyima Lema dhamana.
Namshukuru sana Mwenyezi Mungu, Jamhuri ilikusudia mabaya kwangu lakini Mungu alikusudia mema kwetu, vilevile namshukuru sana mke wangu, kama ningepata fursa ya kuoa tena ningemuoa yeye.. Nikisema niongee ninachotaka kuongea, leo sitaweza, nimeandaa waraka kwa ajili ya mheshimiwa Rais na nitautoa huo waraka hivi karibuni katika siku ambayo tutawatangazia. Nimeona mateso mengi ya watu, mambo mengi ambayo nafasi hii haitoshi.

UCHAMBUZI KUHUSU TOFAUTI KATI YA WASICHANA NA WANAWAKE

1. Wasichana wanatafuta wanaume wenye pesa ila Wanawake wanatafuta wanaume wanaojali na kupenda.
2. Wasichana hupima thamani ya wanaume wao kwa kuangalia ukubwa wa mifuko yao ila Wanawake hupima thamani ya wanaume wao kwa kuangalia kiwango cha busara na hofu ya mungu na kwa vipi wanajiheshimu mbele ya wapenzi wao.


3. Wasichana huvunja mahusiano kwa sabubu zisizo na mashiko ila Wanawake wana uvumilivu wakifahamu kwamba kila jambo hutokea kwa sababu.


4. Wasichana hufikilia kuhusu mambo yaliyopo sasa ila Wanawake hufikilia kuhusu yajayo.


5. Wasichana wanapenda kuwa na wanaume wengi wanaowafuata ila Wanawake wanafahamu sheria ya uhitaji (Vitu rahisi vina wateja wengi).


6. Wasichana wanahitaji pesa ili kununua make-ups ila Wanawake wanahitaji pesa kwa ajili ya kufanyia mipango ya maendeleo.


7. Wasichana huumizwa na mwanaume mmoja na kuwa na kinyongo na wanaume wote ila Wanawake wanajua kwamba wanaume wote sio sawa.


8. Msichana "anajifunza" ila Mwanamke "anajua"

Wednesday, 1 March 2017

POMBE KALI KATIKA VIFUNGASHO VYA PLASTIKI (VIROBA) YAPIGWA MARUFUKU KUANZIA MACHI 1,2017


Mtakumbuka tarehe 20 Februari 2017 Ofisi ya Makamu wa Rais ilitoa tamko la Serikali la utaratibu utakaotumika kutekeleza agizo la kusitisha utengenezaji, uuzaji na matumizi ya pombe kali zinazofungashwa kwenye vifungashio vya plastiki (viroba)kuanzia tarehe 1 Machi 2017.

Utekelezaji wa katazo hili utazingatia Ibara ya 8(1) (b) na 14, Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 na Kanuni zake zilizotungwa kupitia kifungu 230 (2) (f) cha sheria hiyo, na Sheria ya Leseni za Vileo Namba 28 ya mwaka 1968 pamoja na marekebisho yake ya mwaka 2012.

Napenda kusisitiza na kuujulisha umma wa Tanzania kuwa utekelezaji wa maamuzi haya ya Serikali kuhusu usitishaji uingizaji, uzalishaji, uuzaji na matumizi ya vifungashio vya plastiki vya kufungia pombe kali utaanza rasmi tarehe 01 Machi, 2017, katika Mikoa yote ya Tanzania Bara.

Operesheni ya kukagua utekelezaji wa agizo la serikali la usitishaji utengenezaji, uuzaji na matumizi ya pombe zinazofungashwa kwenye vifungashio vya plastiki itaendeshwa nchini kote kuanzia tarehe 2 Machi 2017 kwa kupitia Kamati za Ulinzi na Usalama na Kamati za Mazingira katika ngazi ya Mkoa, Wilaya, Tarafa, Kata, Vijiji na Mtaa.

Kamati hizi zitawajibika kuwasilisha taarifa za operesheni wakati na baada ya operesheni hiyo Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na nakala Ofisi ya Makamu wa Rais.

Mnamo terehe 24 Februari 2017, kiliitishwa kikao cha Mawaziri na viongozi wa taasisi za Serikali kujadili mpango wa utekelezaji wa zuio hili. Katika kikao hicho, Wizara na taasisi za Serikali zilipewa majukumu mbalimbali, kama ifuatavyo:

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kwa kuzingatia umuhimu wa ujazo katika utozaji kodi, imeanzisha mfumo wa stempu za Kielektroniki ili kudhibiti ujazo wakati wa uzalishaji kwa ajili ya kupata mapato stahiki. Aidha, Mamlaka itahakikisha kwamba wazalishaji na waingizaji nchini wa malighafi ya pombe kali (ethanol) wamesajiliwa na kwamba mfumo wa ufuatiliaji wa usambazaji malighafi hiyo unawekwa.

Wazalishaji na waingizaji wa malighafi hiyo watawauzia wale tu ambao wamepewa kibali na pia watatakiwa kutoa taarifa kila baada ya miezi mitatu (3) ya kiasi cha ujazo kilichouzwa na wateja waliouziwa ambao wamesajiliwa. Uuzaji wa malighafi kwa watengezaji wa pombe kali ambao hawajasajiliwa itakuwa ni kosa la jinai kulingana na Sheria.

Mkemia Mkuu wa Serikali ambaye ndiye msajili wa kemikali za viwandani na majumbani, atasajili makampuni na taasisi zinazoingiza kemikali za viwandani na majumbani nchini ikiwa ni pamoja na Ethanol.

Msajili atawajibika kutoa taarifa sahihi za majina ya makampuni na watu binafsi na taasisi zinazohusika, kiasi kilichoingizwa na kimetumika, pamoja na madhumuni ya matumizi.

Kulingana na sheria ya Leseni ya Vileo Na 28 ya Mwaka 1968 na marekebisho yake ya mwaka 2012, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa katika operesheni hii itaratibu zoezi hili katika mikoa, wilaya, tarafa, kata, vijiji na mitaa yote Tanzania bara kwa kuhakikisha kuwa wanaofanya biashara ya pombe ya kawaida na pombe kali (spirit) na watumiaji kinyume na masharti ya leseni za vileo wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kupitia Shirika la Viwango Tanzania (TBS), katika operesheni hii watakukagua viwanda vyote vinavyojihusisha na uzalishaji wa vileo na vifungashio vya aina mbalimbali vya kufungia pombe kali kama vimekidhi viwango vya kitaifa Ukaguzi katika viwanda vya plastiki utachunguza kama kuna mitambo ya kuzalisha vifungashio vya plastiki kwa ajili ya pombe kali.

Mitambo ya kuzalisha vifungashio vya plastiki kama haitumiki kwa kuzalisha bidhaa zingine katika kiwanda husika, mwenye kiwanda atalazimika kutoa ufafanuzi wa hatima ya mitambo hiyo. Mitambo ya kuzalisha vifungashio vya plastiki itakayokutwa inaendelea kuzalisha pombe kali na kufungashia vifungashio vya plastiki itakamatwa na kutaifishwa na wahusika watashtakiwa.

Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Watoto na Wazee, kupitia Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na mabwana afya katika operesheni hii watatoa elimu kwa umma na kukagua maeneo yote yanayotumika kuhifadhia, kuuza na kusambaza vileo vya aina zote, na kushiriki kukamata vileo ambavyo vipo kinyume cha sheria na kanuni.

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, kupitia Idara ya Habari Maelezo, itasaidia kutoa elimu kwa umma kuhusu suala hili.

Wizara ya Mambo ya Ndani, kupitia Jeshi la Polisi, na vyombo vingine vya ulinzi na usalama, itashiriki katika operesheni, ikiwemo kwenye masuala ya inteligensia.

Ofisi ya Makamu wa Rais na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira, wataratibu operesheni.

Kama tangazo letu la tarehe 20/2/2017 lilivyoonesha muda wa nyongeza unaweza kutolewa kwa wazalishaji halali ambao wataonyesha ushahidi wa kuelekea kuhamia kwenye teknolojia ya chupa, na kwamba watahitaji muda mchache kufanya hivyo, na ambao watatimiza masharti kadhaa na kupata kibali maalum kabla ya tarehe 28/2/2017.

Hadi sasa Serikali imepokea maombi ya wazalishaji 9. Tutangaza kesho iwapo kuna ambao wamekidhi masharti au la. Kanuni za upigaji marufuku pombe hizi zipo tayari.

Pia tumepokea malalamiko kwa wazalishaji wengi kwamba zoezi hili limekuja ghafla na wengine wana malighafi na bidhaa kwenye maghala. Ukweli ni kwamba Serikali ilitoa taarifa Bungeni, kuanzia mwezi Mei 2016, na mara kadhaa baada ya hapo, na rekodi zipo, kuhusu hatua hizi.

Vilevile, taarifa ya Serikali iliyotangaza kupiga marufuku pombe za viroba ziliripotiwa kwa ukubwa stahiki kwenye vyombo vya habari, ikiwemo kwenye ukurasa wa kwanza wa gazeti la Mwananchi, mwezi Agosti 2016.

Katika taarifa zote za nyuma, Serikali ilitangaza kwamba hatua hiyo itaanza tarehe 1 Januari 2017. Hatua hizi zimechelewa kwa miezi miwili.

Iwapo, baada ya taarifa hizo za Serikali, kuna mzalishaji ameagiza malighafi au kutengeneza au kuhifadhi pombe za viroba, au kuchukua mkopo kwa ajili hiyo, atakuwa amefanya hivyo akijua madhara yake.

Mwisho napenda kutoa wito kwa wananchi wote kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa zoezi hili la upigaji marufuku matumizi ya pombe zinazofungashwa katika vifungashio vya plastiki (viroba) kwa kutoa taarifa kwa vyombo husika ili wale wanaozalisha na kuuza au kuhifadhi waweze kuchukuliwa hatua stahiki. Zawadi itatolewa kwa watakaotoa taarifa zitakazowezesha kukamatwa kwa watakaokiuka zuio hili.

OFISI YA MAKAMU WA RAIS
28/02/2017