Friday, 6 January 2017

Mhe.BAKHRESA AANZISHA KIWANDA CHA AZAM DAIRY PRODUCTS ZANZIBAR

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) na Mwenyekiti wa Kampuni ya Azam Group Bw.Said Salim Bakhresa wakikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Mradi wa kiwanda cha uzalishaji wa Maziwa (Azam Dairy Products Ltd.)

Wednesday, 4 January 2017

KESI YA MHE LEMA SASA MAHAKAMA YA RUFAA

Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, leo imeshindwa kusikiliza rufani ya Jamhuri dhidi ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kupinga dhamana yake

Tuesday, 3 January 2017

MADAWA YA KULEVYA SIO UJANJA NI MAJANGA

Nando ni kijana aliyeshiriki big brother mwaka 2013, kama mwakilishi wa Tanzania, kutokana na hali ngumu ya maisha kijana huyu alijidumbukiza kwenye janga kubwa la matumizi ya madawa ya kulevya Kwa sasa hali ya Afya ya Nando si nzuri imezorota kutoakana na matumizi ya madawa ya kulevya yaliyokithiri. Hii iwe kama kengele kwa vijana wa kisasa kuwa dawa za kulevya sio “ujanja” ni majanga
Wakati huo huo hali ya mwanamuziki Chid Benzi nayo imerudia kuwa mbaya baada ya kusemekana amerudia kutumia madawa ya kulevya hata baada ya kuwa katika kituo cha REHABILITATION huko Bagamoyo

UMOJA WA MATAIFA WAPATA VIONGOZI WAPYA

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa mhe. Antonio Guterres kutoka Ureno
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa mhe Amina Mohammed kutoka Nigeria, nafasi ambayo iliwahi kushikiliwa na mhe Asha Rose Migiro wa Tanzania

Monday, 2 January 2017

KINADADA MNAOPENDA WENYE "SIX PACKS"

Imetokea hivi karibuni kuwa kama fashion,kina dada kuhangaika kuwa na mahusiano na wanaume waliojengeka miili yao,kitaalam tunawaita "six packs". Hali hii inaumiza wengine wanaohangaika kujenga hayo maumbile.

Angalisho; SIO KILA MWENYE SIX PACKS anafaa kuwa mume au baba bora, wengine wamejenga hayo ili kutumia kwenye ukabaji,wizi wa nguvu......

MAMBO YA KIJIJINI

Kuishi kijijini inabidi uwe mvumilivu...
😬
Unaenda kuoga unakumbuka umesahau sabuni unaenda kuchukua,unafika bafuni unakuta ng'ombe amekunywa Maji yoteπŸ˜„
Unaenda kuchukua mengine ile kurudi bafuni unakuta mbuzi amekula sabuni yako ya kipande ya Mbuni.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Unachukua maji mengine unaamua uoge tu bila sabuni,kumaliza tu unakuta mbwa kabeba taulo hapo sasa watu wote wameshaenda shambani kazi ipo.

Sunday, 1 January 2017

TANESCO YA KWANZA KUTUMBULIWA MWAKA MPYA

Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba

MHE RAIS MAGUFULI ASEMA BEI YA UMEME HAITAPANDA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewahakikishia Watanzania kuwa licha ya Mamlaka ya udhibiti wa huduma za Nishati, Maji na Mafuta (EWURA) kuridhia ombi la TANESCO la kupandisha bei ya umeme kuanzia Januari mosi,2017 bei ya umeme haitapanda.

Rais Dkt. Magufuli amezungumza hayo leo Jumapili ya Januari Mosi, 2016 wakati wa Ibada katika Kanisa la Bikira Maria Mama Mwenye Huruma,Kanisa Kuu Jimbo Katoliki la Bukoba anapoanza rasmi ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Kagera.

Rais Magufuli ameshangazwa na kitendo cha watendaji waliopandisha bei ya umeme bila hata ya kushauriana na yeye, Makamu wa Rais,Waziri Mkuu au Waziri mwenye dhamana ya Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo na hivyo kumshukuru Waziri Muhongo kwa kutengua maamuzi hayo.

''Ninamshukuru sana Waziri wa Nishati na Madini kwa maamuzi ya kusitisha hayo kwa hiyo umeme hakuna kupanda bei,haiwezekani unapanga mikakati ya kujenga viwanda na hasa katika mikakati mikubwa ya nchi ya kusambaza umeme mpaka vijijini,na umeme huu unaenda kwa watu masikini walioumbwa kwa mfano wa Mungu halafu mtu pekee kwa sababu ya cheo chake anapandisha bei,hili haliwezekani'' Alisema Rais Dkt. Magufuli.'

Aidha, Rais Dkt Magufuli ameendelea kuwataka watanzania katika mwaka huu mpya 2017 kuendelea kufanya kazi kwa bidii kama maandiko matakatifu yanavyoelekeza kuwa asiyefanya kazi na asile badala ya kulalamika kuwa fedha zimepotea.

Kwa upande wake,Askofu Msaidizi Jimbo Katoliki la Bukoba,Askofu Methodius Kilaini,akitoa mahubiri kwa waumini waliohudhuria ibada hiyo amempongeza Rais Dkt Magufuli kwa uongozi wake imara,huku akisema kupungua kwa urasimu katika ofisi za umma kunatokana na utendaji kuongezeka na kuwataka wana Kagera na Watanzania kwa ujumla kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kufanya kazi kwa bidii na uaminifu.
Mara baada ya Ibada ya Misa Takatifu iliyoongozwa na Askofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba,Askofu Desderius Rwoma,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli aliwatakia heri ya mwaka mpya waumini wa kanisa hilo na watanzania kwa ujumla.

Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Kagera.
01 Januari, 2017