Friday, 29 April 2016

JIJINI DAR HAKA NAKO NI "KAJIPU UPELE"

Kufuatia uchafuzi mkubwa wa Mazingira Jijini Dar na penginepo nchini, katika kipindi hiki cha mvua hali ya kitaro kuziba imekuwa kitu cha kawaida. Tunaomba hatua zichukuliwe kutumbua haka kajipu upele

MHE RAIS MAGUFULI AFUNGA KIKAO KAZI CHA MAKAMANDA WA POLISI NCHINI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makamanda wa Polisi wa mikoa mara baada ya kufungua kikao kazi chao katika ukumbi wa Dodoma Convention Center mjini Dodoma.

MVUA HIZI HAZITAKI KUTUMBULIWA: HAMENI MABONDENI

Msemo unaojiri mjini kwa sasa ni kuwa Mvua nazo zinawajibika kunyesha kikamilifu kwa kuogopa kutumbuliwa. Ni muhimu kwa wale wanaoishi sehemu hatarishi kutafakari mara mbili maana japo ni hali ya maisha imepelekea waishi huko lakini kwa madhara ya mvua hii pia hali za maisha yao zinazidi kuwa mbaya.

JINSI YA KUUKARIBISHA NA KUUKUMBATIA UMASKINI

🏽
1. Kamwe usiamke mapema, endelea kulala na
kujinyosha mpaka pale njaa itakapokuuma.
2. Kamwe usipange jinsi ya kutumia pesa zako,
wewe zitumie tu pale unapozipata. Na zikiisha
kaa chini na jifikirie umezitumiaje.
3. Kamwe
usifikiri juu ya ku 'save' pesa zako, subiri mpaka
uwe nazo nyingi ndio uanze ku 'save', utasave
vipi pesa zako wakati unazo kidogo?
Wanaokuambia usevu pesa hawakutakii mema
katika matumizi yako.
4. Kamwe usijiingize katika biashara ambazo
huwa mnaziita 'za wasiosoma' wewe ni mhitimu
wa chuo kikuu ulie soma bhana utafanyaje
biashara ya viazi? Utauzaje duka? Utauzaje viatu
vya mitumba? Hizo ni biashara za wasioenda
shule. Wewe unapaswa ukae ofisini upigwe na
kiyoyozi.
5. Kamwe usifikiri kuanzisha biashara mpaka
pale Malaika atakaposhuka toka mbinguni
kukuletea mtaji wa kuanzia biashara.
Watakuambiaje uwekeze wakati hujapata hata
Milioni? Hata kama wafanyabiashara wengi kama
kina bakheresa walianza kuuza mgahawa, wewe
ni smart, unatakiwa uanze na mamilioni katika
biashara zako.
6. Lalamika kuhusu kila kitu,
isipokuwa usilalamike kuhusu uvivu wako na
attitude yako. Ilaumu serikali ya Magufuli,
zilaumu benki zilizogoma kukukopesha fedha,
zilaumu kampuni mbalimbali ambazo zimekutosa
kwenye ajira. Wote hao wana roho mbaya
hawataki kukufanya uwe tajiri!
7. Tumia pesa nyingi tofauti na unachokipata.
Kufanikisha hili nunua bidhaa za kutumia kwa
mkopo, azima pesa kwa washkaji nunua kitanda
cha Milioni moja, nunua Brand new LG flat
screen, pendezesha kwako. Kopa pesa benki
nunua Verossa, watoto wa mjini wakukome.
8. Shindana katika kuvaa. Hakikisha unavaa kila
aina ya fashion mpya ya nguo. Nunua kila aina
ya simu mpya inayotoka, kama ulinunua sumsung
galaxy S6 kwa milioni moja, uza hata laki sita
halaf ongezea hela ukanunue sumsung galaxy
S7. Zimetengenezwa kwa ajili yetu
bhana.Ukishindwa kununua gari mpya, nunua gari
ya mtumba ambayo gharama zake za
kulihudumia ni mara mbili ya mshahara
unaoupata, au gari linalokaa muda mrefu gereji
kuliko barabarani.
9.Wape wanao kila wanachokitaka kwa kuwa
wewe ni mzazi bora, hawatakiwi kuhangaika wala
kufundishwa utu na thamani ya pesa,
usiwafundishe juu ya kutunza na kuheshimu
fedha. Usiwafuatilie kabisa katika masomo yao.
Waache wakue wakiwa wavivu na waje kuwa
masikini kuhakikisha kuwa hawawezi kukusaidia
pale utakapozeeka.
10. Tembelea viwanja vyote vya bata, na uzuri
wamiliki wa maeneo ya starehe wanatujali yaani
wanafungua maeneo mapya kila siku, tembelea
yote. Kula bata kula bata, Nakwambiaje We
Kulaaa Bataa. Na ukishahakikisha kwamba
unatekeleza hayo yote, kaa chini na utafakari
kuwa siku zote fainali nzuri huchezwa uzeeni!
Ponda raha kufa kwaja!
UMASIKINI MWEMA.

Thursday, 28 April 2016

WABUNGE WASIOCHANGIA BUNGENI KUBANWA

Kiti cha Spika wa Bunge kimesema ipo haja ya kufanya marekebisho ya Sheria pamoja na Kanuni ili kila mbunge apate posho kulingana na kazi aliyofanya bungeni, badala ya utaratibu wa sasa wa kuangalia mahudhurio pekee.

Aidha, kimewataka wabunge kubadilika na kuacha tabia ya kuchukua posho za vikao vya Bunge bila kuzitolea jasho.

Kauli hiyo imekuja kutokana na Mwongozo ulioombwa Aprili 25, mwaka huu na Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (CCM) ambaye alikitaka kiti cha Spika kutoa Mwongozo kuhusu usahihi wa wabunge wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kulipwa posho na mishahara wakati hawashiriki na kutimiza wajibu wao wa kuchangia kwenye mjadala wa Bunge la Bajeti linaloendelea katika Mkutano wa Tatu wa Bunge la 11.

Bashe alisema mbunge huyo alitumia Kanuni ya 68(7) ya Kanuni za Kudumu za Bunge akiomba Mwongozo wa Spika kutokana na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, kuamua kutoshiriki mjadala unaoendelea bungeni, lakini wabunge hao wanasaini na kulipwa mishahara na posho.

Hivyo akaomba Mwongozo endapo ni haki kwa wabunge hao kupokea posho wakati hawashiriki wala kutimiza wajibu wao wa kisheria.

Katika kujenga hoja hiyo, Bashe alitumia Ibara ya 63(3) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania isemayo, “Kwa madhumuni ya utekelezaji wa madaraka yake Bunge laweza kujadili utekelezaji wa kila Wizara wakati wa Mkutano wa Bunge wa kila mwaka wa bajeti.”

Aidha, Bashe alitumia Ibara ya 73 ya Katiba ya Tanzania kufafanua kuhusu malipo ya mshahara, posho na malipo mengine kwa wabunge.

Akitoa Mwongozo wa Spika, Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson alisema kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania, Ibara ya 73 imeainisha masharti ya kazi ya wabunge.

Alisema mbunge anastahili kulipwa mshahara kwa kila mwezi, na kufafanua kuwa mbunge anapohudhuria vikao bungeni na kamati atalipwa posho ya vikao kwa kiwango kitakachowekwa na Serikali na Kanuni za Bunge.

Alisema malipo ya mshahara ni suala la Kikatiba na Sheria hulipwa kwa mbunge kutokana na kazi yake ya ubunge.

Hivyo malipo ya posho kwa wabunge yanatokana na mahudhurio yao bungeni na siyo kwa kuchangia kama ambavyo wengi wao wanapenda iwe hivyo.

“Kimsingi kuhudhuria bungeni pekee siyo njia inayopendeza kwa kuwa mbunge anapofika bungeni anatarajiwa atekeleze majukumu yake yalivyoainishwa katika Ibara ya 63.

“…Tabia hii ya kutochangia mijadala na kuzunguka zunguka bungeni haikubaliki na haitakiwi kuendelea, kila mbunge atekeleze wajibu wake na sio anahudhuria ili alipwe posho,” alisema Dk Ackson.

HARAKATI ZA MAENDELEO YA MIUNDOMBINU

Haijapata kutokea, nchi yetu ndani ya siku saba, kuwa na hakika ya kuanza kwa miradi mikubwa miwili yenye kuvuka mipaka ya nchi yetu; mradi wa bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanga, na wa reli ya kati hadi Rwanda na Burundi.
Naamini zama hizi za Magufuli tutashuhudia ujenzi zaidi wa miundo mbinu na kukamilika kwa wakati. Miradi mikubwa ya ujenzi huinua uchumi wa nchi ikiwamo kutoa ajira mpya. Ndivyo ilivyokuwa Ujerumani na kwengineko duniani.

MAFURIKO YAITIKISHA WILAYA YA MOSHI-KILIMANJARO

Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akizungumza jambo na wataalamu alioongozana nao katika uwanja mdogo wa ndege wa Moshi kwa ajili ya kuruka na ndege ndo ya Shirika la Hifadhi za taifa (TANAPA) kwa ajili ya kujionea hali ya mafuriko.

Wednesday, 27 April 2016

MHE. ZITTO KABWE: "CCM NI ILE ILE....."

Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amefunguka na kusema Chama Cha Mapinduzi CCM ni kile kile cha siku zote, Zitto Kabwe amesema hayo baada ya kusoma vitabu vya Bajeti ya mwaka huu na kusema kuwa bajeti hiyo ni ya kulipa deni la Taifa.

Kwa Mujibu wa Zitto Kabwe amedai kuwa Serikali inatarajia kukusanya shilingi trilion 17 kwa mwaka na kusema zaidi ya tirioni 8 zitakwenda kulipa deni la Taifa ambalo ni zaidi ya asilimia 50 ya bajeti na kusema ukichanganya na mishahara ya watumishi ambayo huwa ni nusu ya bajeti ni dhahiri kwamba makusanyo ya Serikali yataishia kulipa madeni na wafanyakazi.

"Nimemaliza kusoma vitabu vya Bajeti ya mwaka huu. Kimsingi ni Bajeti ya kulipa Deni la Taifa.

Wakati Serikali inatarajia kukusanya shilingi trilion 17 mwaka huu, shiling trilioni 8 ikiwa ni asilimia 50 italipia Deni la Taifa. Ukiweka na mishahara ya watumishi ambayo huwa ni nusu ya bajeti, ina maana makusanyo yote ya Serikali yatalipia madeni na mishahara.

Ndiyo maana Serikali inaenda kukopa zaidi ya shilingi trilion 7 mwaka huu na kutegemea misaada ya wafadhili kwa shilingi trilion 5. CCM ni ile ile, ile ile....." aliandika Zitto Kabwe

MAMA MARIA NYERERE ATEMBELEA DARAJA LA NYERERE - KIGAMBONI

Mama Maria Nyerere akifuatana na mwanae Mhe.Makongoro Nyerere na Msaidizi wake wametembelea Daraja la Nyerere ambapo ameonyesha furaha yake kuwa Ndoto ya Baba wa Taifa imetimia- Licha ya mvua kubwa ilokuwa yaendelea lea Jijini Dar, mama huyu aliamua kufika Darajani hapo

Tuesday, 26 April 2016

WABUNI MBINU ZA KUSAFIRISHA BANGI NA MIRUNGI LAKINI WAKAMATIKA

Polisi Mkoani Kilimanjaro imewanasa watu walokuwa na shehena ya Mirungi na misokoto ya Bangi wakiisafirisha kutoka nchi jirani ya Kenya kuingiza Arusha Tanzania. Tazama walivyojipack utadhani mabomu ya kujitoa muhanga

TAYARI UCHAFU HADHARANI DARAJA JIPYA LA NYERERE KIGAMBONI

Hata wiki haijapita tangu daraja hili lifunguliwe rasmi, tayari wananchi wameanza kuchafua mazingira kwa kuweka viroba vya uchafu kwenye nguzo za taa. Tubadilike jamani.

Sunday, 24 April 2016

MWALIMU NYERERE NA SOKA LA TANZANIA

Mwalimu Nyerere alikuwa mpenzi sana wa Soka la Tanzania, hadi pale mwaka 1972 Timu ya Soka ya Tanzania ilipoingia uwanjani bila tshirt na kukaguliwa na kusalimiana na Rais wa Sudan Mhe. Jaffar Mohammad el Nimeiry. Tangu siku hiyo akapoteza moyo wa kuwa shabiki mzuri wa Soka kwa kufedheheshwa na tukio lile

Saturday, 23 April 2016

MTOTO WA KIKE WA KITANZANIA ATIA FORA UMOJA WA MATAIFA


Mtoto Mtanzania mwenye umri wa miaka 16 Getrude Clement kutokea Mwanza amehutubia mbele ya viongozi mbalimbali wa dunia kwenye mkutano wa umoja wa mataifa akiwa mwenye kujiamini na kutoonekana kuwa na hofu japo anaongea kwenye jukwaa ambalo linatazamwa na viongozi mbalimbali.

Mataifa zaidi ya 150 yalitia saini makubaliano ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ikiwemo Marekani ambapo katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki moon ndio alimkaribisha Getrude kuongea kwa kusema ‘ni furaha yangu kumualika Getrude Clement ambaye pia ni mwakilishi wa vijana anayeishi Tanzania na anaziwakilisha sauti za vijana‘

Getrude alianza kwa kuwasalimia waalikwa huku ikiripotiwa Maraisi 60 walihudhuria na kisha akaeleza kuwawakilisha vijana na watoto ambapo alizungumzia mabadiliko ya tabia nchi, hatari yake na kwamba wamekua wakifikisha ujumbe kwa Wananchi juu ya mabadiliko hayo kama anavyoonekana kwenye hii video hapo juu

KINADADA WA KITANZANIA KWANINI HAMJIKUBALI?

Binadamu tumeumbwa kwa sura na mfano wa Muumba (Kwa imani za kidini). Ni kawaida kwa kinadada kujiremba na kujitunza maana ndio silka yao. Lakini unapozidisha kujiremba unageuka kituko maana Waafrika kwa ngozi zetu tunapendeza sana.
Tazama dada huyu anavyopendeza (Natural is beautiful)
Ila kwa hii hapa comment wewe mwenyewe, mie sipooooo....

MALKIA ELIZABETH II WA UINGEREZA ATIMIZA MIAKA 90 YA KUZALIWA

Tar 21 Aprili 2016, Malkia Elizabeth II wa Uingereza aliadhimisha Miaka 90 ya kuzaliwa. Huyu ni Malkia aliyedumu muda mrefu katika kiti hicho cha Umalkia. Alizaliwa 21 Aprili 1926, akawa Malkia wa Uingereza kuanzia mwaka 1952

Thursday, 21 April 2016

MHE RAIS MAGUFULI AWASHUKURU VIONGOZI WA NGAZI MBALIMBALI CCM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akizungumza na Viongozi wa mikoa na wilaya wa Chama Cha Mapinduzi kutoka Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar ambapo aliwashukuru kwa kazi nzuri waliofanya kipindi cha uchaguzi na kuwataka kuwa wamoja na kukiimarisha Chama

MREMA AENDELEA KUOMBA MHE RAIS MAGUFULI AMPE KAZI ILI AMSAIDIE KUTUMBUA MAJIPU

Mwenyekiti wa taifa wa Chama cha TLP na aliyekuwa mgombea Ubunge wa jimbo la Vunjo, Agustino Mrema anatarajia kusafiri kuja jijini Dar es salaam kwa lengo la kumpongeza Rais Magufuli na kumkumbusha ahadi aliyompa mwaka jana ya kumpatia kazi Serikalini.

Akizungumza kupitia kipindi cha Sun Rise kinachoruka kupitia Times fm, Mrema amempongeza Rais kwa jitihada za ukusanyaji kodi na kupambana na Ufisadi kwa nguvu.

“Tuweke itikadi pembeni Rais wa sasa anaweka juhudi katika kukusanya kodi, na mimi nilikuwa napiga nalo sana kelele hili swala, ila akipewa ushirikiano baada ya miaka mitano tutasheherekea mafanikio yake.

“Wiki ijayo natarajia kuja Dar, na nafikiri nitaonana na Rais kwanza nimpongeze alafu nimsisitize anipe nafasi kuna sehemu nazijua tuzisafishe, siwezi kusema mpaka nionane nae ndio nitamueleza”

Wednesday, 20 April 2016

MHA:ASKOFU MATHIAS ISUJA WA JIMBO KATOLIKI DODOMA AZIKWA

Mhashamu Askofu Isuja enzi za uhai wake

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole Askofu Mkuu wa Jimbo la Dodoma , Beatus Kinyaiya katika mazishi ya Askofu Mstaafu wa Dodoma Mathias Isuja yaliyofanyika kwenye kanisa kuu la Mtakatifu Paul wa Msalaba Mjini Dodoma Aprili 20, 2016.
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameongoza maelfu ya waumini na wakazi wa mkoa wa Dodoma katika mazishi ya Mhashamu Askofu Mstaafu, Mathias Isuja wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dodoma.

Amesema kifo hicho ni pigo kwa watu wote na si kwa kanisa pekee kwa sababu walimtegemea kulisaidia Taifa kiroho na kimaendeleo.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatano, Aprili 20, 2016) wakati akizungumza na waumini na wakazi wa mkoa huo na mikoa jirani kwenye ibada ya mazishi iliyofanyika kwenye Kanisa la Kiaskofu la Mtume Paulo wa Msalaba mjini Dodoma.

Askofu Isuja ambaye alizaliwa Agosti 14, 1929 alikuwa Askofu wa kwanza mzalendo katika Jimbo la Kanisa Katoliki la Dodoma. Alistaafu kazi ya uaskofu mwaka 2004 kwa mujibu wa sheria ya kanisa. Alifariki Aprili 13, mwaka huu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka shada la maua kwenye kaburi la Askofu Mstaafu wa Jimbo Kuu la Dodoma, Mathias Isuja katika mazishi yaliyofanyika kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Paul wa Msalaba, Aprili 20, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Tuesday, 19 April 2016

DARAJA LA KIGAMBONI LAZINDULIWA RASMI: KUITWA DARAJA LA NYERERE

Daraja hilo lilipokuwa hatua za mwisho za ujenzi
Mhe Rais John Magufuli akikata utepe kuashiria kufungua rasmi Daraja hili ambalo amependekeza liitwe daraja la Nyerere.

Monday, 18 April 2016

MICHEZO ASILIA YA NYUMBANI

Je upi umeucheza sana?
Bao (Limezoeleka sana mazingira ya Pwani na Zanzibar)
Mdako (Mchezo huu hupendwa zaidi na watoto wakike)