Tazama namna ushirikina unavyoleta ukatili dhidi ya ubinadamu.
Friday, 31 October 2014
Thursday, 30 October 2014
TUCHAPE KAZI ILA KWA UMAKINI
Chombo hiki kinachosaidia kuingiza kipato hakika hakitumiki vizuri. Kama kweli wahitaji kipato endelevu, jali na tunza pia kifaa cha kazi.
SIMANZI ZAMBIA
Ni juzi tu wamesherehekea miaka 50 ya Uhuru wa nchi yao, ila jana Zambia imempoteza Rais wao Mhe. Sata huko London alipokuwa akipata matibabu. Habari zinasema Makamu wa Rais Mhe. Dk, Guy Scottambaye ni wa asili ya Kizungu ndio anashika madaraka mpaka uchaguzi utakapofanyika tena. RIP Rais wa Zambia.
Mhe. Dk. Guy Scott
Mhe. Dk. Guy Scott
UTANI MWINGINE WAHITAJI UJASIRI
Watoto wana namna nyingi za kufanya matani ila matani mengine yahitaji ujasiri mkubwa kuyakubali . Hapa huyu mtoto akiamua kufanya majaribio ya matumizi ya hilo panga, anafungua bucha. Tuwafundishe watoto wetu matani mazuri na yafaayo katika kujijenga binafsi na jamii. Ila pia tuwakumbushe matani mengine ambayo yanaweza kuleta madhara.
UBUNIFU
Katika kuboresha maisha na kuleta mvuto zaidi kimazingira, ubunifu ni muhimu.
Ubunifu katika michezo
Ubunifu katika michezo
Tuesday, 28 October 2014
MISAADA ISIVYOTUMIKA VIZURI
Hivi kweli tuliomba msaada wa net kujikinga na malaria au kuzikinga mboga zetu na malaria au wanyama/ndefu/wadudu waharibifu?
Monday, 27 October 2014
KUMEKUCHA TUKAWAJIBIKE
Tulikotoka ni mbali , pengine asubuhi hii ndo unapasha ugali moto ule uwahi majukumu yako kama ni shule au kazini. Yote maisha, twende tukawajibike.
Tukauze mitumba sasa Gulioni
Nawe Boda boda usijali, hii ni zaidi ya Mshkaki
Mavuno ya mshambani nayo
Tukauze mitumba sasa Gulioni
Nawe Boda boda usijali, hii ni zaidi ya Mshkaki
Mavuno ya mshambani nayo
Sunday, 26 October 2014
UHUSIANO KATI YA TANZANIA NA CHINA WAZIDI KUIMARIKA
Mhe.Rais Jakaya Kikwete akiangalia mchoro wa ramani ya Tanzania unayoonyesha Reli ya Kati inayotarajiwa kufanyiwa ukarabati mpya na wa kisasa na Kampuni ya China, alipokuwa ziarani China wiki hii. Ukarabati huo utahusisha Reli ya kati ya Dar es Salaam-Kigoma, Tabora-Mwanza, Kaliua-Mpanda-Ziwa Tanganyika
Mhe.Rais Kikwete akisalimiana na mwenyeji wake Rais wa China mhe. Xi Jinping
Mhe.Rais Kikwete akisalimiana na mwenyeji wake Rais wa China mhe. Xi Jinping
Thursday, 23 October 2014
Monday, 20 October 2014
MAPENZI YA MUNGU: FILAMU YA LULU NA MAMA KANUMBA
Mwezi, Wiki na Sasa siku zimebaki kwa ile Filamu Mpya na ya Kusisimua ya MAPENZI YA MUNGU Kuingia Sokoni ambayo imewakutanisha wasanii mahiri wa hapa hapa Tanzania ambapo Mmoja kati ya Wasanii waliocheza filamu hiyo Ni Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya anayejulikana kama Linah Sanga, kwa Kushirikiana na Elizabeth Michael LULU bila Kumsahau Flora Mtegoha ambae ni Mama Mzazi wa Marehemu Steven Kanumba watakuwa ndani ya filamu Mpya iitwayo MAPENZI YA MUNGU...Ni Filamu ambayo Kisa chake
na Mafunzo yake yanasisimua lakini Pia ni Moja kati ya filamu ambayo kiukweli ina hadhi na vigezo vya kimataifa...... Nimefika hapa leo sio kwa Ujanja wangu Bali ni Kwa "Mapenzi ya Mungu..."
Filamu ya "Mapenzi ya Mungu" ni moja ya filamu ambayo Msanii Linah pamoja na Mama Mzazi wa Marehemu Kanumba wameonyesha uwezo wa hali ya juu na kuthibitisha kuwa kweli Sanaa ni Kazi.
Filamu ya "Mapenzi ya Mungu" itakuwa Sokoni Kuanzi Wiki hii Kwa Wauzaji wa Filamu kote Nchini.
Filamu hii itasambazwa na Kampuni mahiri ya Proin Promotions Ltd.

MAAJABU YA MTI TABORA
Pichani ni mti unaodaiwa kunyanyuka ghafla baada ya kuanguka miaka mitatu iliyopitakatika kijiji cha Mfuto kata ya Ufuluma ,ambapo wilaya ya Uyui mkoani Tabora.
Katika hali ya kushangaza huku kila mtu akifikiria yake baaya ya juzi huko mkoani Tabora, kutokea tukio la aina yake ambapo inaelezwa kuwa mti aina ya Msufi uliokuwa umeanguka yapata miaka mitatu iliyopita umesimama ghafla tena kwa sauti kubwa ya mrindimo na kuwafanya wananchi kujitokeza kwa wingi kushuhudia tukio hilo.

EBOLA YALETA HOFU MWANZA
Watu sita wakiwamo wahudumu watatu wa afya wa hospitali teule ya Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza, wamewekwa chini ya uangalizi maalum baada ya kumhudumia mgonjwa aliyefariki akiwa na dalili za ugonjwa wa ebola.Mtu aliyefariki alitajwa kuwa ni Salome Richard (17), anayetoka katika kijiji cha Kahunda wilayani Sengerema.
Akithibitisha kuwapo kwa hali hiyo Mganga Mfawidhi wa Hospitali Teule ya Wilaya ya Sengerema, Dk. Mary Jose, alisema mgonjwa huyo alifikishwa katika hospitali hiyo na ndugu zake watatu akiwa na homa kali huku akitokwa na damu sehemu mbalimbali za mwili wake.Alisema vipimo vya mgonjwa huyo vimepelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili na Nairobi Kenya kwa uchunguzi zaidi.

Sunday, 19 October 2014
Saturday, 18 October 2014
TULIOKATAA VIJIJI VYA UJAMAA,MNASEMAJE HAPA
Nyumba 38 zilizojengwa karibu kabisa na makao makuu ya wilaya ya Uyui huko Isikzya Tabora.Ni katika mpango mzima wa mradi wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu.
WHEN IN ROME,DO AS ROMANS DO" UKIWA ROMA ISHI KAMA WAROMA WANAVYOISHI
Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe.Anna Makinda akiwa Muscat kwa ziara rasmi za Kibunge
Mhe.Spika akiwa na ujumbe wake alipokutana na wenyeji wake huko Muskat. Shela/hijab inahusu!
Mhe.Spika akiwa na ujumbe wake alipokutana na wenyeji wake huko Muskat. Shela/hijab inahusu!
Friday, 17 October 2014
WAMEPENDEZAJE?
Ni ijumaa, wiki ya masomo imeisha kwa shule za msingi. Basi wao wanarudi nyumbani wakiwa wametokelezea kivyao. Hapana chezea fashion wewe.
BUSARA YA LEO: MAMBO YA KUJITAHIDI KUFANYA KABLA YA KUFIKIA MIAKA 30
1. Tambua uwepo wa Mungu na jitahidi kuzingatia maadili ya imani yako.
2. Jifunze kuweka akiba ya fedha tena bila kuigusa aidha benki au taasisi za fedha
3. Tafuta mpenzi sahihi na tulia nae kupanga maisha
4. Ishi mahali pa peke yako, sio kukaa na washkaji au mashoga tu
5. Lipa madeni yako ya zamani yote. Pia watake radhi mliokosana, jenga amani na watu.
6. Jenga mwili wako na jitahidi kutunza afya yako.
7. Jitahidi kuwa na marafiki wanaokujenga na kukupa changamoto za kimaendeleo za maisha.
8. Anza kuweka vitega uchumi kama kununua ardhi, biashara n.k
9. Jitahidi kuvaa kwa heshima sio ili mradi tu. Kata K na vimini sio dili
10.Tambua na ukubali kuwa umekua na uache tabia za kitoto au kufuata mkumbo.
11.Yaache ya zamani yapite na uanze upya.

Thursday, 16 October 2014
CCM NA WOSIA WA BABA
Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa CCM kwenye ukumbi wa NEC,CCM Makao Makuu Dodoma.
MELI KUBWA KULIKO ZOTE DUNIANI KWA SASA
Meli ya Oasis Seas ndio inayoongoza kwa ukubwa. Ina uwezo wa kuchukua abiria 6,300 na wahudumu 2394 kutoka zaidi ya nchi 71. Ndani ina kila aina ya maraha. Imetia nanga katika Bandari ya Southampton huko Uingereza.
Ramani ya meli hiyo
Ramani ya meli hiyo
Wednesday, 15 October 2014
UTAALAMU WA HALI YA JUU WA TANESCO NA TANROAD
Nguzo hii ya Umeme ipo barabarani maeneo fulani huko Mbeya. Sasa sijui wahusika ndo wameona hapo ndo utaalamu wao wote umetumika hadi kufanya hivyo au hawaona kama kuna tatizo
NGUO ZA JESHI WAACHIE WANAJESHI
Raia huyu alikutwa na adha hiyo maeneo ya Kariakoo baada ya kukutwa amevaa majazi ya jeshi ilihali yeye si mwanajeshi
Tuesday, 14 October 2014
NYERERE DAY
WATANZANIA leo tunaadhimisha kumbukumbu ya miaka 15 tangu kufariki kwa muasisi na Rais wa kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Mwalimu Nyerere alifariki dunia Oktoba 14, 1999 akiwa nchini Uingereza alipokuwa amelazwa akisumbuliwa na maradhi ya kansa ya damu.
Maadhimisho ya siku hii kitaifa yamefanyika huko Tabora sambamba na sherehe za kuzima Mwenge mgeni rasmi akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe Jakaya Mrisho Kikwete
Juu ni picha wakati wa siku za maombolezo ya kifo cha Baba wa Taifa mwaka 1999
Kiongozi wa mbio za Mwenge mwaka huu ndg Rachel Kassandra akimkabishi mhe,Rais Kikwete mwenge wakati wa kilele cha mbio hizo huko Tabora
Makamanda wa Mwenge wa Uhuru