Wednesday, 30 July 2014

HONGERA RAIS WETU MHE. J KIKWETE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kwa mara nyingine ametunukiwa tuzo ya kimataifa – zamu hii kwa kuwa mshindi waTuzo la Nyota wa Demokrasia Afrika 2014 – Icon of Democracy Award Winner for 2014 in Africa

HONGERA DIAMOND PLATNUMZ

Diamond Platnumz akionesha tuzo yake aliyoshinda kwa baadhi ya vyombo vya habari na mashabiki waliofika kumlaki,mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere leo asubuhi (30.7.2014) kutokea Marekani ambako alishinda zawadi ya Mwanamuziki bora wa kiume wa Afrika Mashariki 2014.

Tuesday, 29 July 2014

EID MUBARAK WADAU

Umati wa waamini wa kiislam waliohudhuria swala ya Eid el Fitr huko uwanja wa Maisara Zanzibar
Viongozi wa Serikali na dini waliohudhuria swala hiyo
Swala ya Idd el fitr katika Masgid Maamur Upanga Dar
Swala na mawaidha katika uwanja wa Mnazi Mmoja Dar

ENZI ZA MWALIMU......

Enzi za Mwalimu Nyerere hizi zilikuwa pesa halali na zenye thamani kubwa. Leo zimebaki kuwa urembo tu. Ipi tathmini ya thamani ya fedha yetu?

VIONGOZI VIJANA MHE. JOSHUA NASSARI NA STEPHEN MASELE KUKUTANA NA MHE.RAISI OBAMA LEO

Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Mhe Joshua Nassari akizungumza wakati wa tafrija ya chakula cha jioni baada ya mahafali ya kuhitimu mafunzo ya wiki tisa kwa viongozi vijana toka nchi mbalimbali za Afrika yaliyokuwa yakifanyika chuo kikuu cha Arkansas nchini Marekani
Ukumbi ambapo Mhe raisi Obama atazungumza na Vijana viongozi wa Afrika wanaoonyesha dira (the most promising young African leaders)

Sunday, 27 July 2014

NAKUMATT MLIMANI CITY YAFUNGULIWA RASMI LEO

Kampuni ya Nakumatt Holdings leo imeanza kutoa huduma katika duka lililopo Mlimani City Dar baada ya kuchukua maduka hayo ya Shoprite ya Afrika Kusini.
Wafanyakazi wa kwanza wa Nakumatt Mlimani City wakiwa na furaha ya kuanza kazi

UNYENYEKEVU WA KIONGOZI MKUU WA KANISA KATOLIKI

Baba Mtakatifu Francis 1 akipokea huduma ya chakula katika moja ya migahawa huko Roma.

Saturday, 26 July 2014

MRADI MKUBWA WA COCO BEACH PARK

TIB Development Bank ikishirkiana na Uongozi wa Manispaa ya Kinondoni umefanya upembuzi yakinifu na kuandaa mchoro wa kuendeleza fukwe hizo maalum jijini Dar

SERIKALI YAIFUNGIA HOSPITALI YA IMTU-MBEZI AFRICANA DAR

Serikali imeifungia Hospitali ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba na Teknolojia (IMTU), baada ya kuifanyia ukaguzi na kubaini kasoro kadhaa za uendeshaji wake.
Ukaguzi huo ulifanywa jana na jopo la wataalamu kutoka Manispaa ya Kinondoni, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, baada ya IMTU kukumbwa na kashfa ya utupaji wa mabaki ya viungo vya binadamu katika Bonde la Mto Mpiji, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.
Ukaguzi huo ulifanywa jana na jopo la wataalamu kutoka Manispaa ya Kinondoni, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, baada ya IMTU kukumbwa na kashfa ya utupaji wa mabaki ya viungo vya binadamu katika Bonde la Mto Mpiji, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.
Hospitali hiyo imefungiwa wakati Kamati ya Watu 15, iliyoundwa na Serikali ikiendelea kuchunguza kashfa hiyo

Friday, 25 July 2014

UJENZI WA BARABARA ZA JUU(FLY-OVER) KUTIWA SAHIHI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) na Balozi wa Japan nchini Masaki Okada (kulia) wakibadilishana hati ya makubaliano ya mikataba miwili ya ujenzi wa barabara za juu kwa juu katika makutano ya TAZARA na usambazaji umeme jijini Dar es salaam leo zenye thamani ya zaidi ya bilioni 128.

KAAAZI KWELIKWELI!!!!!

Unakula msosi huu.......,halafu unakutana na kibarua hiki......

SIKU YA MASHUJAA TANZANIA YAFANA-VIWANJA VYA MNAZI MMOJA DAR

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipokea salama ya Heshima mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini dar es Salaam jana katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa
Kwa mbali ni jengo jipya karibu na Jengo la Ushirika ambalo miaka ya nyuma ndilo lilikuwa jengo refu maeneo hayo

AIR ALGERIE YAENDELEZA MACHUNGU YA MAJANGA YA NDEGE

Wakati bado ulimwengu waomboleza vifo vya watu 298 walioangamia kwa kudunguliwa ndege ya Malaysia,na pia ile ajali ya ndege ya Taiwan, Ndege ya Air Algerie aliyoanguka huko Mali ni janga kubwa kwa Afrika na Ulimwengu. Watu wote 116 waliokuwa katika ndege hiyo wamepoteza maisha jangwani.Ndege hiyo ilikuwa safarini kutoka BurkinaFaso kwenda Algeria.
Hii ni mojawapo ya ndege ya shirika la Air Algerie
Mabaki ya ndege hiyo iliyoanguka Jangwani na kuungua. Inasemekana Majeshi ya Ufaransa yalotumwa kuitafuta ndege hiyo yamefanikiwa kupata kinasa sauti na matukio ya ndege hiyo (Black Box). Wengi wa waliopoteza maisha katika ndege hiyo ni raia wa Ufaransa.

Tuesday, 22 July 2014

DOUBLE TREE BY HILTON YAPIGA HODI ZANZIBAR

Kampuni kubwa ya Hilton na Double Tree by Hilton imetangaza kufungua Hoteli Mpya ya kisasa ya vyumba 58 huko StoneTown Zanzibar. Tayari wana Hotel ya Double Tree by Hilton Dar es Salaam eneo la Msasani karibu na The Slipway.

Saturday, 19 July 2014

HII HAIKUBALIKI

Japokuwa usingizi ni ubinadamu,lakini huu ni uzembe na kutokuwajibika.

Friday, 18 July 2014

NAFASI ZA MASOMO WAMA NAKAYAMA SEC.SCHOLL

Zikiwa zimepita siku chache tangu matokeo ya Kidato cha sita kutangazwa. Shule ya Wama-Nakayama inatangaza nafasi za masomo. Wanaopenda kujiunga soma hapa...

HAPO ZAMANI ZA KALEEEEEE

Baba wa Taifa miaka ya ujana wake.
Mdau unajua hiki kiatu kinaitwaje, wakati huo unavaa na bugaloo

Thursday, 17 July 2014

MALAYSIA AIRLINE MAJANGA TENA

Ndege nyingine ya Shirika la Ndege la Malaysia,imeanguka mpakani mwa Ukraine na Urusi na inasadikiwa watu wote waliokuwemo wamefariki. Ndege hiyo MH17 ilikuwa inatokea Amsterdam Uholanzi kwenda Kuala Lumpur ikiwa na abiria 280 na wafanyakazi 15
njia ya ndege hiyo na mahali ilipopoteza mawasiliano
Picha zaidi za tukio