Friday, 8 April 2011

MAMBO YA LOLIONDO

Baada ya Babu Ambilikile kuendelea kutoa tiba kwa kutumia kikombe kimoja cha maji wameanza kuzuka watu wengine katika sehemu mbalimbali za TZ wakidai nao wamepewa maono ya kutibu watu kwa kutumia dawa kama afanyavyo babu. Je tumwamini yupi?

Sunday, 6 February 2011

BUTIAMA NA MAKUMBUSHO YA BABA WA TAIFA MWL.J.K. NYERERE











1.Hili ni jumba la Makumbusho ya Mwalimu J.K.Nyerere, Butiama mkoani Mara.
2.Picha mbali mbali za Mwalimu enzi za uhai wake.
3.Redio aliyokuwa akiitumia kwa ajili ya kusikiliza habari mbalimbali alipenda pia kuitumia katika baadhi ya ziara zake za ndani na nje ya nchi. Redio hii alipewa zawadi huko Ujerumani mwaka 1969.

4.Hivi ni baadhi ya viatu alivyokuwa akivaa Hayati Mwalimu J.K.Nyerere. Mwalimu alipenda zaidi viatu vya kutumbukiza, pembeni kama mkoba ni redio yake. Itizame kwa uzuri katika picha inayofuata.

5.Urithi wa asili wab Tamaduni za kizanaki silaha za jadi, vifaa vya nyumbani, ala za muziki, mapambo ya asili, lugha, mila, desturi - nk. Vyte utavikuta kwenye nyumba hii ya makumbusho ya Mwalimu.

6.A gift of traditional stool given to Mwl. Nyerere by the residents of Dar-es-Salaam after the victory of Kagera war in 1978 - 1979.
7.Joho la Uhitimu.

8.Jiwe la kusagia nafaka huitwa 'Ombwe' na dogo huitwa Esyo, kwa kawaida kazi ya kusaga hufanywa na wanawake. Chakula kikuu cha wazanaki ni ugali, huliwa kwa nyama, samaki na mboga za majani. (Picha:Mdau Mwanza)

TUJIPANGE KUANZA VIZURI WIKI YA KAZI


Weekend imeisha sasa, si vibaya tukijipanga tena vizuri kuanza wiki inayoanza vizuri, kuweka mipangilio yenye kuleta mafanikio, kuongeza uvumilivu katika magumu tutakayokumbana nayo na kujitahidi kutafuta mbunu mbalimbali za kurahisisha maisha kwa njia sahihi. Nawatakieni wadau wote wiki njema.

Saturday, 5 February 2011

Noti Mpya Zimechakachuliwa: Gavana Ndulu

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imekiri kuwa noti mpya ilizozitoa kuanzia mwezi uliopita zimeanza ‘kuchakachuliwa’ na wahalifu kwa kutengeneza noti bandia.

TUMECHOKA KUGONGWA NA MAGARI


Mwanafunzi wa darasa la sita katika Shule ya Msingi Oysterbay,Dar es Salaam, Rashid Omary, akisimamisha magari ili wanafunzi wenzake wavuke katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi eneo la Oysterbay. Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani,Mohamend Mpinga ameuzindua mfumo huo wa wanafunzi kujivusha wenyewe.Picha na Hassan Mndeme wa Jeshi la Polisi