www.mkandamizaji.blogspot.comKaribuni wadau kwenye kiwanja kipya hicho.
Monday, 31 August 2009
MASANJA WA ORIJINO KOMEDI KWENYE BLOG
Masanja nae kaibuka kwenye blog na amekuja na kitu kinaenda kwa jina la
MWISHO WA MWEZI
Mwisho wa mwezi umewadia, tunapoganga yaliyopita,pengine picha hii inaweza kukukumbusha mengi. Zingatia kusamehe waliochukizwa na mafanikio yako, na jitahidi kuimarisha mafanikio uliyopata mwezi mzima,na yawe kichocheo cha mwezi ujao. Jitahidi kupunguza wakuchukiao kwa kuwa "mtu wa watu", na pengine kwa kuweka mipaka.
Nawatakieni nyote Mwisho mwema wa mwezi na mwanzo mwema wa wiki.
Nawatakieni nyote Mwisho mwema wa mwezi na mwanzo mwema wa wiki.
Sunday, 30 August 2009
WADAU NAWATAKIENI JUMAPILI NJEMA
Saturday, 29 August 2009
NOTI MPYA YA SHILINGI 2,000
BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa noti mpya za Sh2,000 ambazo zitatumika sanjari na zilizopo kwenye mzunguko kwa sasa.
Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu alisema jana kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari kwamba, lengo la kutoa noti hizo mpya ni kukidhi mahitaji yake kwenye mzunguko wa fedha nchini.
"Noti hizi mpya zinatofauti moja tu na zile ambazo zimo kwenye mzunguko kwa sasa nayo ni saini zilizopo.
Saini zilizopo kwenye noti mpya ni za Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo na Gavana wa Benki kuu ya Tanzania,” alisema.
Profesa Ndulu alisema kuwa noti hizo bado zina rangi ya kahawia, zikiwa na michoro inayoonyesha mandhari ya kitanzania kiuchumi, kiutamaduni pamoja na urithi wetu na mazingira.
"Mbele ya noti, bado kuna picha inayoonyesha utajiri wetu wa kuwa na mojawapo ya wanyama pori wakubwa yaani simba ,alama ya kificho ya twiga ambayo bado ipo kama ilivyo katika noti nyingine zinazozunguka sasa" lilifafanua tangazo hilo.
Alama nyingine zilizopo katika noti hiyo ambazo hazina tofauti na iliyopo kwenye mzunguko ni nyuma ya noti kuna picha inayoonyesha picha ya ngome kongwe illiyopo Forodhani jijini Zanzibar.
Vile vile, alisema zina picha ya kinyago cha kuchonga na alama ya usalama inayobadilika rangi ikigeuzwa.
”Benki kuu inawashauri wananchi kuwa hakuna haja ya kubadili noti hizo kwani thamani yake ni ileile na kwamba haina mpango wa kuzifuta zilizokuwepo katika mzunguko wa awali.
Habari imeandikwa na Burhani Yakub wa gazeti la Mwananchi.
Friday, 28 August 2009
USALAMA WA MABASI YA ABIRIA:Yote kufungwa mikanda
Akizungumza jijini Dar es salaam jana, Kombe alisema suala la kufunga mikanda katika mabasi sio jambo la hiari na halina mjadala ni wajibu wa kila mmiliki wa basi kuhakikisha anatekeleza agizo hilo kwani ni moja ya sheria za usalama barabarani nchini.
Alisema ifikapo Oktoba mosi basi ambalo litakuwa halijatekeleza agizo hilo litakamatwa na askari na kupelekwa mahakamani pamoja na kulizuia kuendelea kufanya kazi hiyo ya kusafirisha abiria.
Amesema jeshi hilo limejipanga vizuri kukabiliana na mabasi ambayo hayatatekeleza agizo hilo na watapewa adhabu kali kwa kudharau agizo hilo.
Amesema lengo la agizo hilo ni kukabiliana na ajali za barabarani zimalizike ama zitoweke kabisa na kila basi linatakiwa liwe na cheses nzuri, na mikanda ya kuvaa abiria wanapokaa kwenye siti kwa kuwa abiria wamekuwa wakijeruhiwa na kufa kwa kukosekana kwa mikanda hiyo
MUITE AKUPAMBIE NA KUIPENDEZESHA SHEREHE YAKO
Thursday, 27 August 2009
UREMBO WAHITAJI UVUMILIVU SANA
Kinadada wanapenda sana urembo ikiwa ni mojawapo na kusuka nywele. Kuna mtindo wa ususi wa nywele unaopendwa sana, ila wasusi wake maarufu ni jamii ya Kimasai. Style hii ya ususi inawataka kinadada hawa wakae kitako muda mrefu na ili kazi hii iweze kuisha mapema kidogo inabidi wasusi wawe wawili. Hapa dada huyu anachoka kukaa,kuinamisha shingo na kuna mengine kama "kajismell" toka kwa hawa jamaa na pengine pia suala la "mfadhaiko". Hongera kinadada kwa uvumilivu wenu.
Wednesday, 26 August 2009
NANI ALAUMIWE?
Wadau,leo ngoja niongelee tabia ya "KULALAMIKA" bila kuchunguza zaidi nani wa kulalamikiwa na nini sababu ya kulalamika.
Katika picha hizi mbili hapa chini:
Mama huyu mfanyabiashara wa khanga na vitenge,ameuchapa usingizi katika eneo la biashara yake. Si ajabu mwisho wa siku akifanya mahesabu ya mapato yake kwa siku ataanza kulalamika "oooh siku hizi wateja hakuna, biashara haichanganyi, Rais hatuangalii watu wake,viongozi wazembe, njaa sana,nchi ya tabu sana hii" na maneno mengine kama hayo. Lakini sidhani kama katika tathmini yake ya kufanya biashara alizingatia vigezo ya biashara. Kwa mfano,mazingira anapofanyia biashara pana mwelekeo wa kuvuta wateja?, kauli yake kwa wateja je?, bei za bidhaa?, aina za bidhaa na mengine kama hayo. Zaidi sasa tunapoangalia picha hii, ni ukweli kwamba sidhani kama wateja watavutwa kuja kununua kitu kwako wakati wewe umelala, muda utakaotumia kuamka, kujiweka sawa na kuanza kuhudumia mteje tayari atakuwa keshakereka. Tusibaki tunalaumu tu,tuangalie hayo.
Katika picha hii nayo tunamwona jamaa huyu,yaonekana nae ni mfanyabiashara au mfanyakazi katika gari. Yeye kaona sehemu ya kupumzikia ni chini ya gari, tena gari lenyewe laonekana halina break imara ndio maana wameweka jiwe karibu na tairi.Lakini kiutaalamu uzito/egemeo la gari na uzito/egemeo la hilo jiwe haviendani. Hapo atakuwa amelalamika weeeeee kwamba hali ya maisha ngumu hadi amepata usingizi. Kwa mfano kama ni gari la kubeba mchanga hata mteja akija na kukuta amelala hivyo ni vigumu sana kumwamsha maana mteja unapokuja unategemea upokelewe kwa shangwe na maneno ya mvuto,"Mteja ni Mfalme" Halafu pia kwa bahati mbaya likitokea la kutokea labda gari limebiringika,ndio kusema hapo lazima watu waandae nyimbo za maombolezo.
Haya na mengine mengi ni ya kuangalia badala ya kulalamika tu.

Picha kwa hisani ya www.samvande.blogspot.com
Tuesday, 25 August 2009
HII KALI ZAIDI
Monday, 24 August 2009
NAWATAKIENI WIKI NJEMA
Ni jumatatu tena,mwanzo wa pilikapilika za juma. Nae mwanamama huyu yupo katika pitapita za kutafuta maisha. Jua ni kali na maisha ndio hivyo tena.Kizuri ni kwamba anamjali sana mwanae hadi anatafuta namna ya kumkinga na jua. Hongereni kinamama kwa malezi na matunzo sahihi.Tuongeze bidii katika majukumu yetu,maisha yataboreka tu japo si kwa siku moja.
Wakati kila mmoja akiwa anajibiidisha kutafuta riziki, Mwombaji Maarufu Mzee Matonya ambaye aliondolewa jijini Dar,sasa kahamia katika mitaa ya Mji wa Morogoro akiendelea na mbinu yake ya kutafuta pesa ili kusukuma gurudumu la maisha.

Sunday, 23 August 2009
MISS UNIVERSE 2009
Mrembo wa dunia kwa mwaka 2009 anatoka Venezuela kwa mara nyingine. Huyu ni Stefania Fernandez.Mwaka jana 2008 Mrembo wa Dunia alikuwa Dayana Mendoza nae pia kutoka Venezuela.Mrembo wetu Illuminata kwa bahati mbaya hata kwenye 15 bora hakuwepo lakini,labda bado wakati wa kuwapta warembo kutoka Tanzania japo ni warembo sana.
Miss Universe 2009 Stefania Fernandez
Miss Universe 2008 Dayana Mendoza
Miss Universe 2009 Stefania Fernandez
Miss Universe 2008 Dayana Mendoza
MOTO WATEKETEZA BWENI IRINGA
BWENI LA SHULE YA SEKONDARI YA IDODI YA MKOANI IRINGA, LIMETEKETEA KWA MOTO NA WANAFAUNZI WAPATAO 14 WAMEFARIKI DUNIA KATIKA TUKIO HILO LILILOTOKEA USIKU WA KUAMKIA LEO. KWA MUJIBU WA MWANDISHI WETU ALIYEFIKA ENEO LA TUKIO, AJALI HIYO ILISABABISHWA NA MSHUMAA AMBAO ULIWASHWA NA MWANAFUNZI MMOJA ALIYEKUWA AKIJISOMEA USIKI NA KWA BAHATI MBAYA ALIUSAHAU KUUZIMA HADI UKAWASHA GODORO. HABARI ZAIDI ZINASEMA HUENDA IDADI YA WALIOFARIKI IKAONGEZEKA, KWANI HADI SASA WANAFUNZI WAWILI HAWAJULIKANI WALIPO. NI AJALI NYINGINE MBAYA YA MOTO KUTOKEA SHULENI AMBAYO INAWAKUMBUSHA WATU ILE AJALI MBAYA KULIKO ZOTE YA 'MOTO WA SHAURITANGA'!
JUMAPILI NJEMA
Saturday, 22 August 2009
MAMBO YA "SUMMER TIME"
Mke wa rais wa Marekani Barack Obama, Michelle Obama amezidi kuonyesha tofauti yake na wake wa marais waliopita wa Marekani. Michelle amekuwa mke wa kwanza wa rais kuvaa kikaptula na kupanda dege la rais Air Force One walipokuwa katika mapumziko na ziara fupi huko Arizona. Taswira hii imepewa maelezo tofautitofauti
MFUNGO MTUKUFU - RAMADHAN KAREEM
Friday, 21 August 2009
WATOTO KATIKA NCHI YA SHIBE
Pamoja na ukweli kuwa nchi yetu imebarikiwa katika mambo mengi, bado hali ya maisha ni ngumu kwa wengi.Chakula ni cha kubangaiza na hata wakati mwingine baadhi ya jamii zinalazimika kuokota chakula toka majalalani. Hali hii inapaswa kufikia tamati. Hata hivyo, hili ni jukumu la Taifa zima si viongozi peke yao.
Wednesday, 19 August 2009
MSIBA JIMBO KUU KATOLIKI MWANZA-ASKOFU MKUU MAYALLA
ASKOFU mkuu wa jimbo kuu la Mwanza, Kanisa Katoliki Mhashamu Anthony Petro Mayalla (69) amefariki dunia leo mchana kutokana na maradhi ya moyo baada ya kuugua ghafla akiwa ofisini kwake.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na mkurungenzi wa mawasiliano wa baraza la Maaskofu (TEC) kanisa katoliki, Padri Revocatus.Makonge Askofu huyo amefariki baada ya madaktari wa Hospitali ya rufaa ya Bugando kuhangaika kumpatia matibabu bila ya mafanikio.
Alisema kuwa marehemu aliamuka salama leo na kuendelea na shughuli zake za kila siku ofisini kwake mpaka majira ya saa 4:00 asubuhi ambapo alizidiwa ghafla na kukimbizwa Hospitali ya rufaa ya Bugando.Habari kutoka katika ofisi ya aksofu huyo, zimeeleza kuwa alipatwa na maradhi hayo wakati akiwa katika maandalizi ya ziara ya waziri wa mambo ya nje wa Vatican ambaye alikuwa akitarajiwa kufanya ziara jimboni kwake Oktoba 5 mwaka huu kwa ajili ya kufungua ujenzi wa hospitali ya watoto.“Baada ya kufikisha hospitalini hapo madaktari waliahangaika kuokoa maisha yake lakini nahati mbaya lifariki dunia majira ya saa 8;30 mchana,” alieleza Padri Revocatus Makonge.
Askofu Mayalla alizaliwa Aprili 23 mwaka 1940 katika katika kijiji cha Nera wilayani Kwimba na kupata elimu yake ya msingi katika wilaya hiyo na masomo ya sekondari.Askofu Mayalla alikuwa amehitimu shahada ya kwanza ya elimu aliyopita katika chuo kikuu cha Loyola huko Chicago Marekani mwaka 1973 hadi 1975
BAADA YA "FAKE PASTOR", SASA NI "VILLAGE PASTOR"
Tuesday, 18 August 2009
JAMANI TUMEZIDI SANA KUONGOZWA NA VIONJO
ZOMBE NA WENZAKE SASA HURU
Watuhumiwa wakipanda kwenye gari la Polisi baada ya kuachiwa huru kuepa vurugu za wananchi
Gari lililomchukua Zombe likitoka katika eneo la Mahakama baada ya Mashtaka kufutwa
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam,jana ilitoa hukumu ya kushtusha baada ya kumwaachilia huru aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP), Abdallah Zombe na wenzake wanane waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya mauaji ya wafanyabiashara watatu na dereva teksi mmoja.
Akisoma hukumu hiyo iliyochukua zaidi ya saa sita, Jaji wa Mahakama ya Rufani,Salum Massati, alisema baada ya kupitia ushahidi na vielelezo vilivyowasilishwa mahakamani hapo, amebaini kuwa serikali imeshindwa kuthibitisha mashitaka hayo
Maelezo haya ni kwa hisani ya Na Happiness Katabazi
Monday, 17 August 2009
WIKI IMEANZA: Nawatakieni wiki njema.
Tunataka kuvuka ng'ambo tuwahi kazini na kwenye mihangaiko mingine ya Jijini. Lakini swali ni kwamba tutaenea wote kweli.Hizi ni nyakati za MV.Alina.
Kwa sasa tunaipongeza Serikali kwa kutuimarishia usafiri kiasi fulani kwa hii MV.Magogoni ambayo ina uwezo mkubwa tofauti na ile Mv.Alina. Hata hivyo kauli yetu na ombi letu ni kwa Serikali kujitahidi kuweka Daraja la kuunganishi sehemu hizi mbili maana hiyo itasaidia sana suala zima la usafiri na maendeleo pande zote.Maana hata maembe ya "Kibada" yatafika kiurahisi sokoni Kariakoo.