Tuesday 30 June 2009

KUPOKEA NA KUTAFUTA.......

Vijana hawa wanatafuta riziki zao kwa kila namna.


Ukiangalia vizuri utaona noti ya shilingi 1000,yanini kwa huyu mwanafunzi na toka kwa nani?. Mie sina tafsiri zaidi hapa

UJENZI WA DARAJA LA MATOMBO

Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete akisikiliza maelezo juu ya maendeleo ya ujenzi wa Daraja la mto Mtombozi huko Matombo, Morogoro.Wengine ni Ndg. Aggrey Mwanri (TAMISEMI), na Eden Munisi (MKURUGENZI MTENDAJI)

Sunday 28 June 2009

MBILIA BELL KATIKA VIWANJA VYA BUNGE

Mwanamuziki toka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Mbilia Bel akicheza muziki na Spika wa Bunge Mhe.Samwel Sitta wakati alipotumbuiza katika viwanja vya bunge mjini Dodoma jana.
Mwanamuziki toka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Mbilia Bell akitumbuiza katika viwanja vya bunge mjini Dodoma jana.

USAFIRI WA NYUMBANI


Hii ni Nzega Tabora.Usafiri kama huu ni tangu mababu. Kuna haja ya kubadili jamani, maana hata kwa namna fulani haki za wanyama zinakiukwa hapa.

Hii ni "enzi za mwalimu" ambapo Basi kama hili lilitumia siku 3 njiani kutoka sehemu moja hadi nyingine fupi tu.

Leo tuna usafiri huu murua,Kutoka Dar hadi Arusha huku ukijisomea gazeti na soda pembeni, muziki mwanana, full kipupwe n.k.

Baada ya muda tutarajie na haya nayo yaja kwa usafiri wa Ferry - Kigamboni na Mwanza City - Ukerewe hahahahaha

Ila kwa wakati huo huo , kuna huu usafiri mwingine tena unaokuja kwa kasi sana hasa Jijini Dar, sijui ndio ubunifu au....

KILA MTU ATAUCHUKUA MZIGO WAKE MWENYEWE

Lakini jamani, hata kwa hawa????

WATEJA HAKUNA NIFANYEJE?

LEO NI SIKU YA BWANA, ILA "SALINI KILA WAKATI"


"Waacheni watoto wadogo waje kwangu"

Saturday 27 June 2009

SHEIKH SULEIMAN GOROGOSI AMEFARIKI AJALINI

Habari zilizothibitishwa na ndugu wa karibu zinasema kuwa Naibu Mufti wa Tanzania Sheikh Suleiman Gorogosi amefariki kwa ajali ya gari akiwa njiani kutoka kutoka Mtwara kuelekea Lindi.Ajali hii ilisababishwa na kupasuka kwa gurudumu la mbele la gari alilokuwa akisafiria. Habari zaidi baadae...............Mola amweke pema peponi.

WEWE MTOTO WEWEE !

Pii Piii wa MARLAW UPO JUU


Sikiliza upate raha yake

HASHEEM THABEET MAMBO SAFI NBA

KING OF POP APUMZIKE KWA AMANI


Jumba la Michael Jackson

Sehemu ya maombolezo

Enzi za ujana wake

Michael Jackson akiwa na Dada yake Janeth Jackson akiwa anatoka mahakamani 2003

Umati ukiwa nje ya barabara ya kuelekea nyumbani kwa Michael Jackson

Friday 26 June 2009

MICHAEL JACKSON AFARIKI DUNIA

Habari za hivi punde kadiri ya "The Los Angeles Times" zinasema , Mfalme wa Pop Michael Jackson amefariki huko Los Angeles mara baada ya kufikishwa hospitalin hapo akiwa mahututi. Hii ni baada ya kupata mshtuko wa moyo (cardiac arrest) mchana wa jana. Habari zaidi baadae..........Hapa ni Michael Jackson akiwa na Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi alipotembelea Tanzania miaka ya tisini

Uh!

POKEENI VITANDA NA MAGODORO HAYA LAKINI SI KULALA TU; SOMENI KWA BIDII

Mwenyekiti wa WAMA ambaye pia ni Mke wa Rais wa Tanzania Mama Salma Kikwete akiwakabidhi Shule ya Sekondari Maginga ilioko Kibaha Mkoa wa Pwani.Vifaa hivyo vimetolewa na Stanbic Bank

Wednesday 24 June 2009

UHANDSOME USHINDWE MWENYEWE: NENDA Chocolate Princes Boutique

Bango la Chocolate Princes Boutique likiwa linawekwa kabla ua ufunguzi rasmi leo jijini Dar.Duka hili lipo Mikocheni karibu na Kwa Mwalimu kwenye maduka mapya katika jengo maarufu la 'Talk of Town' katika barabara iendayo Rose Garden.Mmiliki Mboni Masimba, anasema "uhandsome" unaanzia hapo hivyo kinababa/kinakaka karibuni.

Upendeleo maalum wahamia kwa wanaume sasa

Sehemu iliyosheheni viatu vya kila aina na rangi toka Italy. Kwa maelezo zaidi toka kwa mmiliki mpigie tu kupitia namba +255 773 787 272

Ehee KANUMBA, ULISEMA NANI HANA MVUTO,KANENEPEANA..........?

"NIKIPATA NAULI" wa MPOTO feat BANANA

TABASAMU: MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA

JK AKUTANA NA WAKURUGENZI WA ZAIN,TIGO NA ZANTEL


Rais Jakaya Kikwete akizungumza na Wakurugenzi Watendaji wa mitandao ya simu za mikononi za Zain, Zantel na Tigo. kutoka kushoto ni bwana Nabil Tofilis wa Zantel, Pablo Guardia Vasquez wa Tigo na Khaled Muhtadi wa Zain

Monday 22 June 2009

TAARAB YAMPOTEZA NYOTA NASMA KHAMIS


Mwimbaji mahiri na aliyewahi kutamba sana kwenye anga ya muziki wa taarabu hapa nchini, Bibie Nasma Khamis wa Kidogo ( pichani) amefariki dunia usiku wa kumkia leo.
Baba mdogo wa Marehemu ambaye amejitambulisha kwa jina la Mzee Kaniki akizungumza na vyombo vya habari nyumbani kwake Kinondoni Sharif Shamba ambako ndiko msiba uliko amesema Marehemu alikuwa na matatizo ya shinikizo la damu tatizo lililokuwa likimsumbua mara nyingi, hata hivyo siku za hivi karibuni alishikwa na maralia na kupelekwa katika Hospitali ya Temeke ambako alilazwa na kukaa hapo kwa siku nne mpaka mauti yalipompata usiku wa kuamkia leo
Nasma Khamins atakumbukwa kwa nyimbo zake nyingi nzuri zilizokuwa zikipendwa na mashabiki wengi wa muziki kama vile "Naona mambo iko huku" wimbo uliovuma sana wakati huo akiwa na kundi la muungano kundi hilo likiwa hasimu mkubwa wa kundi lingine la la muziki wa Taarab TOT, ambapo mwimbaji mshindani wa Nasma alikuwa alikuwa Khadija Kopa.
Mungu ailaze mahali pema peponi Roho ya Marehemu Nasma Khamis Kidogo Amin

HABARI KWA HISANI YA www.michuzijr.blogspot.com na www.fullshangwe.blogspot.com

BAADHI YA VITUO VYA MAFUTA BONGO - "WIZI MTUPU"

Picha hii haihusiani na taarifa yenyewe bali ni kiwakilisho tu kuipa nakshi habari


Na Aziza Nangwa

Vituo vitano vya mafuta vimetozwa faini mkoani Ilala kwa makosa ya udanganyifu kwa wateja wanaokwenda kujaza mafuta kwenye vituo hivyo.
Akizungumza na mwananchi ofisini kwake jana meneja wa wakala wa vipimo mkoani Ilala Agustino Maziku, alisema baada ya kukagua vituo 60 vilivyopo mkoani Ilala na waligundua vituo vitano vya mafuta vikikiuka sheria za vipimo kwa kutoa rakiri katika mashine za kupimia mafuta.


Maziku alifanunua kwamba vituo vyote vya mafuta vinakuwa na mashine ambazo ni seals ambazo husaidia mashine hizo kupima mafuta kwa haki bila ya kumpunja mteja lakini zikichezewa huwa na uwezo wa kubadilisha mita za pampu ziweze kutoa mafuta kidogo na huku zikionyesha zimetoa mafuta mengi hivyo kumsababishia mteja asipate kiasi cha mafuta aliyokusudia bila yeye kujua.


“Lazima watu wote wajue sisi kazi yetu ni kusimamia swala zima la kuhakikisha vipimo vinakwenda sawa. Tunahakikisha watu hawapunjani sehemu zote hata kwenye vifungashio vya viwandani wanapima idadi sahihi iliyoandikwa kwenye kifungashio hicho”alisema Maziku
Alisema kuwa sambamba na operesheni hiyo walifanikiwa kamata watu 152 kwenye vizuizi vyao mbalimbali kwa kukiuka ufungashaji bidhaa kwa kutumia kipimo cha lumbesa badala ya ufungaji wa kawaida na waliwatoza faini kila mmoja.


Maziku alisema wamekuwa wakifanya msako wa namna hiyo mara kwa mara kulingana na hali halisi iliyopo na kuwa wamekuwa wakikagua kipimo kimoja kimoja na kutoa taarifa maalumu inayowataka wateja wa eneo husika kuleta mizani yao katika ofisi za watendaji ili vipitiwe na kwamba mtaalamu wa vipimo na anayekiuka anatozwa faini.
Katika operesheni yetu ya hivi karibuni tumekamata jumla ya mizani feki 30 na zingine 24 zilizochezewa ili zisitoe vipimo sahihi 24.


Hata hivyo Maziku alisema changamoto zinazowakabili kwa sasa ni upungufu wa watumishi, vyombo vya usafiri na gharama za uendeshaji zoezi katika idara yake havitoshi kulingana na eneo, magari yaliyopo hayatoshi kwenda kwenye maeneo haraka zaidi.
Pia aliwataka wananchi wenye nia njema washirikiane na ofisi yake ya vipimo kutoa taarifa mara kwa mara pale wanapoona kuna ubabaishaji katika vipimo kwenye maeneo yao.

VODACOM DAR-es-SALAAM MARATHON


Hapa ni Sara Ramadhani toka Zanzibar akishangilia ushindi akiwa anamalizia mbio hizo

Mshindi wa Kwanza wanawake Sara Ramadhani akipokeA ZAWADI toka kwa Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Joel Bendera,(kushoto)Mkurugenzi wa Bodi ya wakurugenzi wa Vodacom Peter Kisumo.

Mshindi wa Mashindano ya Vodacom Dares Salaam Marathon katika mbio za kilometa 21 kwa wanaume Fabian Joseph akishangilia baada ya kumaliza mbio hizo na kuibuka mshindi wa kwanza na kujinyakulia kitita cha shilingi Milioni 1.

Sunday 21 June 2009

TUNAPOELEKEA MACHWEO YA SIKU YA BABA DUNIANI "FATHER'S DAY",..................

Mpendwa,
Nakuomba usichoke kuisoma hadithi hii,inafundisha sana,nawe upate kujifunza kitu katika hadithi hii...Fuata basi na ahsante kwa kuisoma na kutoa maoni wewe waonaje?



Kaka Chongo alikuwa akimchukia sana babake, kisa alikuwa chongo…
Baba yake alikuwa anafanya kazi ya ualimu na kufanya biashara ndogondogo ili kuweza kumtunza mtoto wake pekee. Mtoto ambaye alikuwa akimsomesha shule ya bweni kule Tabora. Baba huyu alikuwa "mjane", mkewe alifariki kwenye ajali ya gari, miaka mingi nyuma....

Siku moja alifunga safari kwenda kumtembelea mtoto wake kule shuleni. Mtoto wake hakufurahia ujio wa Baba yake, na chuki yake ilionekana dhahiri kuwa amechukia.
"Kwanini huyu mwanaume anapenda kuja kuniaibisha kila mara," alijisemea moyoni, dharau zake kwa baba yake na kutojali kwake kulionekana wazi wazi usoni kwake.

Siku ya pili yake mwanafunzi mwenzake darasani alimuuliza… “kumbe wewe Baba yako anajicho moja?” kijana yule akamjibu yule si Baba yangu, ni jirani yetu kule nyumbani...
Kwa kweli hakumpenda Baba yake... alitamani apotelee mbali asimuone tena...
Au afe asiwepo tena duniani...

Baba yake hakumchukia na wala hakuonyesha kisirani kwa mtoto wake…
Kijana yule alisoma kwa bidii sana ili aweze kupata scholarship, ili atakapopata nafasi yakuendelea na masomo ya juu,awe mbali na Baba yake…
Kwa bidii zake alifanikiwa kwenda kusoma nje ya nchi kwa miaka mitatu…

Kwa miaka yote hiyo hakuwahi kuwasiliana na baba yake, na watu wakimuuliza kuhusu wazazi wake aliwajibu kuwa walishafariki siku nyingi…
Baada ya kumaliza masomo nje ya nchi, alirejea nchini na kununua nyumba, akaoa na baada ya miaka michache akapata watoto wawili… Akawa ni mtu mwenye furaha na maisha yake na familia yake…

Siku moja Baba yake ambaye sasa ashakuwa mzee sana, akaja kumtembelea, baada ya kuitafuta nyumba yake kwa takribani siku nne... Baba yake alikuwa ametamani kumuona mwanaye kabla M’Mungu ajamchukuwa… Na pia alitamani kuwaona wajukuu zake…maana alisikia habari hizo.

Alipokuwa akigonga mlango, wakatoka wajukuu zake… walipomuona kibabu kizee chenye jicho moja wakacheka na kumwambia baba yao… kuna omba omba kaja anaonekana ana njaa sana huku wakicheka… Mwanaye alipotoka kumuona huyo omba omba, akagunduwa kuwa si ombaomba bali ni Baba yake mzazi…

Alimwangalia kwa jicho kali na dharau na huku akimkaripia… hivi wewe kizee ujafa tuu…. Na umekuja kufanya nini hapa unatisha watoto wangu… Toka nisikuone hapa hatuna chakula wala pesa za kukupa…. Yule Baba akajibu kwa upole... “Samahani baba nimekosea nyumba nilifikiri hapa anaishi mtoto wangu Fulani…!! Kijana akajibu huna mtoto nyumba hii huna haya weee mzee…!!
Yule Baba huku akilia ndani ya nafsi yake akajiondokea taratibu huku akijikongoja kwa uzee…

Wiki chache kupita, kijana akaletewa barua kutoka kwa wakili wa serikali. Wakili akamtaka aende ofisini kwake. Alipofika na kujitambulisha, wakili akamfahamisha kuwa Baba yake ambaye alikuwa analelewa nyumba ya wazee amefariki siku tatu nyuma. Akampatia na barua kutoka kwa Baba yake. Wakili akashangaa kwani kijana hakuonyesha hata kusikitika…!!
Habari ya kufiwa haikumuuzunisha hata chembe…
Aliporudi nyumbani akajifungia ndani peke yake na kuisoma barua hile...


Kwa mwanangu mpendwa...
Siku zote nilikuwa nakufikiria na kukuombea dua ufanikiwe...
Nakutaka msamaha sana kwa kuja nyumbani kwako na kusababisha kutishika kwa watoto wako, kwa kuwa mimi nilikuwa chongo...!! Na pia nakutaka msamaha kwa vijana wote waliokuwa wakikutania kwa kuwa na Baba ambaye ni chongo...

Mwanangu mpendwa..... Tangu siku ile nilipokuja kwako, nilipata maradhi na sikuweza tena kutoka nje...!! Nawashukuru sana hawa vijana wanaotutunza hapa kwenye nyumba ya wazee...!! kwa kuweza kututunza vyema... Mwanangu mpendwa... kuna jambo moja ambalo nililificha miaka yote hii na leo nimeona nikuandikie hii barua kukufahamisha kile kilicho kuwa ni siri yangu...!!

Japokuwa utapokuwa ukiisoma barua hii... nitakuwa nimeshatangulia kwa Mola wangu...
Ulipokuwa mdogo ulipata ajali mwanangu.... wewe na Mama yako. Mama yako alipoteza maisha kwenye ajali hiyo, na wewe ukapoteza jicho lako moja...

Mimi nikiwa ni Baba yako sikufurahia kukuona ukiwa na jicho moja...
Lakini sikuwa najinsi ya kufanya... Lakini nilijitahidi kutafuta pesa na nikachukua mkopo serikalini nikakupeleka nje ya nchi kufanyiwa operesheni ya jicho...!! Nikakubali kutolewa jicho langu moja kukupa wewe mwanangu ili uione dunia kwa macho mawili… uwe ni mwenye furaha duniani na kukuepusha kuchekwa na watoto wenzio....

Wenzangu walishangaa sana kusikia kuwa nimetoa jicho langu kwa ajili yako mwanangu... lakini najivunia tendo langu hilo kwani ni tendo ambalo limenipa furaha ktk maisha yangu kwa kumwona mwanangu anakuwa na furaha ya kuona ulimwengu akiwa na macho yote.

With my love to you… huo ni urithi pekee nilioweza kukupatia…
Ndimi Baba yako….
Mzee Chongo


Tusiwasahau wote maana hatujui tumetendewa nini mpaka tukafika hatua tuliyo nayo

NI KUSOMA IMEKUWA TABU AU DHARAU!



Na hawa je? Yaani wamekosa sehemu nyingine za kupumzikia wakaona bora relini,mmh!

LEO NI SIKU YA BABA DUNIANI ("FATHER'S DAY")

Leo tunapoadhimisha siku ya Baba Duniani ("Father's Day") , ni wakati mzuri wa kumshukuru Mungu kwa kutupatia Baba duniani. Tuna mengi ya kujivunia na kuwashukuru wazazi wetu au hata walezi wetu. Je, umekumbuka kumkarimu Baba leo?

Kwa upande wangu mie(Mwenye Blog) namshukuru Mungu pia kwa kumwita kwake Baba yetu tarehe 23/03/2009 ambaye leo tungejivunia kuwa nae katika Maadhimisho haya. Shukrani zetu tunazipeleka katika sala tukimwomba Mungu ampumzishe mahali pema, Amina